TANGAZO


Monday, January 14, 2013

Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Zanzibar, Hussein Ibrahim, akabidhi vifaa mbalimbali yakiwemo magari ya wanafunzi, wagonjwa, kuzolea taka, vifaa vya michezo na vya maji

Baadhi ya magari yaliyokabidhiwa na Mwakilishi Hussein Ibrahim Makungu wa Jimbo la Bububu, mjini Unguja, kama alivyoahidi kwa wapiga kura wake wakati wa kampeni.

Baadhi ya matenki ya kuhifadhia maji na mabomba ya kusambaza maji yaliyokabidhiwa na Mwakilishi huyo kama alivyoahidi wakati wa kampeni zake za kuwania Jimbo hilo.

Hussein Ibrahim Makungu, akihutubia wananchi wa Jimbo la Bububu muda mfupi kabla ya kukabidhi magari na vifaa kwa wananchi wa jimbo lake hilo jana.
Vijana wa Jimbo la Bububu wakimshangilia mwakilishi wao, Hussein  Makungu, wakati alipokuwa akiwahutubia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Seif Ali Idd akihutubia kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa maalumu kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya michezo, magari, matenki ya maji nakadhalika, vilivyotolewa na Mwakilishi Hussein Ibrahim Makungu kwa wananchi wa jimbo lake mjini Unguja jana.

Mwanadada akiselebuka kwenye sherehe za kupokea vifaa vya michezo na magari kutoka kwa Mwakilishi Makungu jana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia), akikabidhi funguo za basi la wanafunzi kwa Katibu wa Jimbo la Bububu jana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia), akikabidhi mabomba ya kupitishia maji kwa Jimbo la Bububu jana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd,  akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya Mala FC, Hamad Yahya. Kushoto ni Mwakilishi wa Bububu, Hussein Ibrahim Makungu.
Mamia ya wakazi wa Jimbo la Bububu wakiwa katika hafla hiyo jana. (Picha zote na Martin Kabemba)

No comments:

Post a Comment