TANGAZO


Monday, January 14, 2013

Jaji Mkuu Chande, Spika Makinda waongoza Mahakama na Bunge kutoa Maoni ya Katiba Mpya, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange pia ashiriki

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kulia), akiongea na ujumbe wa Mahakama ukiongozwa na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman (kushoto), uliofika katika Ofisi za Tume, jijini Dar es Salaam leo, Jumatatu, Jan 14, 2013, kuwasilisha maoni ya mhimili huo, wa dola kuhusu Katiba Mpya.
(Picha zote na Tume ya Katiba) 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kushoto) akiongozwa na Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Prof. Mwesiga Baregu kutoka nje ya ukumbi katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya Tume na Mahakama uliolenga kupata maoni ya mhimili huo kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika leo (Jumatatu, Jan 14, 2013).
 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (katikati), akiongea katika mkutano uliolenga kupata maoni ya wadau wa Ulinzi kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na kushoto ni Mjumbe wa Tume na Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, akiongea katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo, Jumatatu, Jan 14, 2013, ambapo mhimili huo wa dola uliwasilisha maoni yake kwa Tume kuhusu Katiba Mpya. Wengine ni watumishi wa Bunge walioongozana naye.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, akitoa maoni ya Bungea kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo, Jumatatu, Jan 14, 2013. Wengine ni watumishi wa Bunge walioongozana naye.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, akiongea katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo, Jumatatu, Jan 14, 2013, ambapo mhimili huo wa dola uliwasilisha maoni yake kwa Tume kuhusu Katiba Mpya. Wengine ni watumishi wa Bunge walioongozana naye.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mohamed Chande Othman (kushoto), akitoa maoni ya Mahakama katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, uliofanyika Ofisi za Tume, jijini Dar es Salaam leo, Jumatatu, Jan 14, 2013. Wengine kutoka kulia ni Wajumbe wa Tume, Makamu Mwenyekiti wa Tume na Jaji Mkuu mstaafu, Augustino Ramadhani, Profesa Mwesiga Baregu, Raya Suleiman Hamad na Jessica Mkuchu.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (wa pili kushoto), na Majaji wengine kutoka Mahakama za Tanzania wakimsikiliza Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Hanifa Masaninga akiwaeleza kuhusu uaandaaji wa maoni ya wananchi na kuwa katika mfumo wa taarifa rasmi (hansard), wakati Majaji hao, walipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo, Jumatatu, Jan 14, 2013.

No comments:

Post a Comment