TANGAZO


Saturday, January 5, 2013

Moto wapamba Tasmania Australia

 
Moto umepamba katika kisiwa cha Tasmania, Australia, na kulazimisha maelfu ya watu kukimbia makwao.
 
Moshi umetanda Tasmania kutoka moto uliozagaa
Moto ulipozidi kuzagaa watu wengi walikimbilia pwani na ilibidi kuokolewa kwa mashua.
Nyumba zaidi ya 100 zimeangamia.
 
Kuna myoto kama 40 inawaka katika kisiwa hicho lakini upepo mkali na joto jingi limeanza kupungua.
 
Wazima moto piya wamekuwa wakipambana na moto barani Australia, ambako joto limezidi katika kiangazi cha mwaka huu.

No comments:

Post a Comment