TANGAZO


Saturday, January 5, 2013

Rais Chavez huenda asiwepo kuapishwa

Bunge la Venezuela litaanza kikao huku wasiwasi ukizidi ikiwa Rais Hugo Chavez ataweza kuanza muhula wake wa pili wa uongozi au la.

 
Rais Hugo Chavez na makamo wake, Nicolas Maduro

Bwana Chavez anauguzwa Cuba baada ya kufanyiwa upasuaji kutoa saratani, na inafikiriwa huenda akawa mgonjwa sana na hataweza kuhudhuria sherehe ya kuapishwa juma lijalo.

Hata hivo makamo wa rais, Nicolas Maduro, alisema Bwana Chavez anaweza kuapishwa baadae mbele ya mahakama makuu, na alikataa wito wa upinzani kwamba kufanywe uchaguzi mwengine.

Mwandishi wa BBC, Sarah Grainger, akiwa mjini Caracas, anasema ufunguzi wa kawaida wa bunge la taifa umekuwa muhimu safari hii kwa sababu ya Bwana Chavez kukosekana.

No comments:

Post a Comment