TANGAZO


Wednesday, January 30, 2013

Mkutano wa mafunzo ya Viwango vya Kimataifa vya ukaguzi wa ndani kwa wakaguzi wa ndani wa Serikali za Mitaa kutoka Halmashauri za Kanda Kati, wafanyika mjini Dodoma, wafunguliwa na Mkaguzi Mkuu Msaidizi wa ndani wa Serikali, Constantine Mashoko

Mkaguzi Mkuu Msaidizi wa ndani wa Serikali katika Serikali za mitaa, Constantine Mashoko akifungua rasmi mkutano wa mafunzo ya viwango vya Kimataifa vya ukaguzi wa ndani leo, mjini Dodoma.
Wakaguzi wa ndani kutoka Kanda ya Kati, wakisikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi leo, mjini Dodoma.
Wakaguzi wa ndani kutoka Kanda ya Kati wakiwa kwenye mkutano wao huo, wakisikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi, mjini Dodoma leo.
Wakaguzi wa ndani kutoka Kanda ya Kati, wakiwa kwenye mkutano wao huo, wakati ukifunguliwa na  Mkaguzi Mkuu Msaidizi wa ndani wa Serikali katika Serikali za mitaa, Constantine Mashoko, mjini Dodoma leo.
Mshauri mwelekezi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Aloyce Maziku akitoa mafunzo ya viwango vya Kimataifa vya Ukaguzi wa Ndani kwa Wakaguzi wa Ndani, mjini Dodoma leo.
Kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi wa Serikali, upande wa Bajeti na mishahara, Stanslaus Mpembe, Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Serikali Msaidizi Constantine Mashoko na Mkuu wa Hazina Ndogo Dodoma, Evance Asenga wakibadilishana mawazo, wakati wa mkutano huo, mjini Dodoma leo.
Kutoka kushoto ni Afisa wa Fedha Mwandamizi, Vicky Jengo, Katibu Muhtasi, Janet Mwamanga, wakiwa kazini katika kufanikisha mkutano huo, ambao pia nao ni washiriki wa mkutano huo.
Baadhi ya Wakaguzi wa Ndani wa Serikali kutoka Halmashauri za Kanda ya Kati wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa rasmi leo. (Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Fedha)

No comments:

Post a Comment