TANGAZO


Friday, January 11, 2013

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Idd, afungua nyumba mpya za Wazee Sebleni, Zanzibar

Nyumba mpya za Wazee, Sebleni zilizofunguliwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi, huko Sebleni, Mkoa wa Mjini Magribi, ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar. (Picha zote na Yussuf Simai-Maelezo, Zanzibar)
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Abdi Mahmoud Mzee, wakati alipowasili kwa ajili ya ufunguzi wa nyumba mpya za Wazee Sebleni, Mjini Zanzibar leo.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi akikata Utepe ili kuzifungua nyumba mpya za wazee, Sebleni, Mkoa wa Mjini Magribi, ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi, akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Fatma Gharib Bilal, wakati akitembelea nyumba mpya za Wazee, Sebleni Mjini Zanzibar leo, mara baada ya kuzifungua rasmi.
Baadhi ya Wazee wa Sebleni, wakimsikiliza Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza baada ya kuzifungua nyumba mpya za Wazee, Sebleni Mjini Zanzibar leo.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi akimpatia funguo za chumba, Mzee Daud Seif Khamis katika nyumba mpya za Wazee, Sebleni Mjini Zanzibar leo, mara baada ya kuzifungua, ikiwa ni katika Shamrashamra za maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi akimpatia Funguo za Chumba, Bi. Tiba Vuai katika nyumba mpya za Wazee, Sebleni Mjini Zanzibar leo, mara baada ya kuzifungua, ikiwa ni katika Shamrashamra za maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi  akiwahutubia Wazee wa nyumba za Sebleni, mara  baada ya kuzifungua nyumba zo mpya, ikiwa ni katika Shamrashamra za maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment