TANGAZO


Friday, January 11, 2013

Vodacom yachezesha droo kubwa ya mwisho ya PATAPATA na Nokia, Wateja 70 waibuka washindi

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani, Dar es Salaam leo, wakati wa kuchezesha droo kubwa ya mwisho ya promosheni ya PATAPATA na Nokia,  iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom pamoja na Nokia, msimu wa Sikukuu. Jumla ya washindi  70, wamepatikana kupitia droo hiyo. Kushoto ni Msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao na kulia ni Meneja Masoko wa Nokia Ellen Lupilli.
Msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao (kushoto), akishuhudia Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa akiongea na mmoja wa washindi, Fidel Ngowi, mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam, kupitia simu ya mezani, wakati wa kuchezesha droo kubwa ya mwisho ya promosheni ya PATAPATA na Nokia,  iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom pamoja na Nokia, msimu wa Sikukuu. Jumla ya washindi  70, wamepatikana kupitia droo hiyo. Anayeshuhudia, kulia ni Meneja Masoko wa Nokia, Ellen Lupilli. 
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati wa kuchezesha droo kubwa ya mwisho ya promosheni ya PATAPATA na Nokia  iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom pamoja na Nokia, msimu wa Sikukuu. Jumla ya washindi  70,  wamepatikana kupitia droo hiyo. Kulia ni Msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao na katikati ni Meneja Masoko wa Nokia, Ellen Lupilli.
Meneja wa Idara ya vifaa vya Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Elihuruma Ngowi (kushoto), akimpigia simu mmoja wa washindi kati ya 70, walioibuka kidedea wakati wa droo kubwa ya mwisho ya promosheni ya PATAPATA na Nokia,  iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom pamoja na Nokia, msimu wa Sikukuu. Jumla ya washindi  70, wamepatikana kupitia droo hiyo. Kulia ni Msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao na katikati ni Meneja Masoko wa Nokia, Ellen Lupilli.

Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam, Januari 11, 2013
WASHINDI takribani 70 wamepatikana kupitia droo kubwa ya Patapata na Nokia Ushinde' ambayo imechezeshwa ikishirikisha wateja wote walionunua bidhaa hizo tangu kuanza kwa promosheni hiyo mnamo mapema mwezi Desemba mwaka 2012.

Katika Droo hiyo iliyoendeshwa na Nokia kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom, wateja 20 wameibuka washindi na kujinyakulia zawadi za simu aina ya Nokia Lumia 900, wengine 20 wamezawadiwa Nokia Lumia 800 huku wengine 30 wakiibuka na Nokia 808.

Miongoni mwa wateja waliopatikana katika droo hiyo ya moja kwa moja ni pamoja na Farhia Hassan mkazi wa Dar es Salaam akiyejinyakulia Nokia Lumia 900, mwingine ni Dennis Katunzi kutoka Mwanza aliyezawadiwa Nokia Lumia 800 huku Fidel Ngowi kutoka Dar es Salaam akipata Nokia 808.
Droo hiyo kuu ya kuhitimisha promoshni hiyo tangu Vodacom na Nokia walipoizindua , imechezeshwa moja kwa moja kwenye Makao Makuu ya Vodacom, Mlimani City, Dar es Salaam, na kusimamiwa na bodi ya michezo ya kubahatisha nchini (Tanzania Gaming Board).

Akizungumza wakati wa promosheni hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Kelvin Twissa, amewataka washindi wengine waliojishindia zawadi mbalimbali na kujulishwa kupitia simu zao za mikononi wafike kuchukua zawadi zao kati ya Januari 11 na 14 katika maduka ya vodacom nchi nzima.
Twissa amefafanua kuwa droo hiyo ambayo imemalizika, imewezesha mteja mmoja mmoja kujipatia muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi 1000 tangu ilipoanza mwezi mmoja uliopita.

Naye Meneja wa Biashara wa Nokia, Ellen Lupilli, amewataka washindi waliopatikana kuwa mabalozi na mashuhuda kwa wengine ambao bado wanamtazamo hasi dhidi ya promosheni kama hizo.

Aidha, amewashukuru watanzania waliojitokeza kwenye promosheni hiyo, ambapo kwa niaba ya Nokia ameahidi kuzidi kuboresha huduma kwa maslahi ya wateja wake.
"Nawasihi wateja wa bidhaa za Nokia kuendelea kuzipenda bidhaa zetu, na zaidi jitokezeni kwa wingi wakati mwingine tunapoandaa promosheni kama hizi, inaweza kuwa bahati yako," amesema Lupilli.

No comments:

Post a Comment