Magari ya moshi mawili yamegongana nchini Afrika Kusini karibu
na mji mkuu wa Pretoria. Takriban watu 100 walijeruhiwa.
"Magari ya moshi yote mawili yalikuwa yamejaa wasafiri ambao husafiri kwenda Pretoria kila siku , wakiwemo watoto wengi tu waliokuwa wanaelekea shuleni," msemaji wa huduma za dharura aliliambia shirika la habari la AFP.
Afrika Kusini inakarabati mtandao wake wa safari za gari moshi ambao umezeeka.
Ajali hiyo ilitokea mapema asubuhi baada ya gari moshi mmoja lilipogongana na lingine lililokuwa limeegeshwa karibi na Attridgeville, kamji kadogo magharibi mwa Pretoria.
No comments:
Post a Comment