TANGAZO


Thursday, November 1, 2012

Warsha ya Wadau wa Sekta ya Maji yafanyika jijini Dar es Salaam

Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa siku mbili unaoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Bluer Pearl jijini Dar es Salaam leo, ambapo warsha hiyo imewakutanisha wadau wa sekta ya maji nchini.

Profesa Maghembe amesema kuwa wanampango wa kuhakikisha kuwa katika kipindi cha malengo ya milenia mpaka kufikia mwaka 2015, asilimia 90 mpaka 98 ya wakazi wanaoishi mijini wanapata maji safi na salama. Ameongeza kuwa malengo ya milenia ni kuhakikisha kuwa asilimia 65 ya wakazi wa vijijini wanapata maji ambapo mpaka sasahivi kwa vijijini tayari wamefikia 58% jambo ambalo wanategemea kuhakikisha kuwa kufikia mwaka 2015 wawe wamefikia malengo hayo.
 
Profesa Maghembe akizungumza na waandishi wa habarri, Dar es Salaam leo mara baada ya kuifungua warsha hiyo.
 
Profesa Maghembe akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa Sekta ya Maji, mara baada ya kuufungua mkutano  wao jijini leo.
 
Wadau waliokuwemo kwenye warsha hiyo wakisikiliza kwa Makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa na waelimishaji kwenye warsha hiyo jijini leo.(Picha zote na Philemon Solomon wa Fullshangwe)
 

No comments:

Post a Comment