TANGAZO


Thursday, November 1, 2012

Ulinzi waimarishwa wakati Sheikh Ponda na wenzake wakifikishwa Mahakamani, Dar es Salaam leo

 

Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, akiwa chin ya ulinzi mkali wa Askari Magereza, wakati yeye na wenzake walipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo kusikilizwa mashtaka yao yanayowakabili. Sheikh Ponda anakabiliwa na kosa la kuvamia kiwanja.
 
Askari Magereza wakiwa katika ulinzi mkali nje ya Mahakama ya Kisutu, walikofikishwa Katibu wa Taasisi na Jumiya za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake kwa ajili ya kusikilizwa kesi yao inayowakabili, Dar es Salaam leo.. 
 
Askari Magereza wakiwa wamevalia mavazi maalum ya kujikinga na shambulizi kota kwa maadui zao, wakati wakiwa katika ulinzi wa kumlinda Shikh Ponda Issa Ponda, wakati yeye na wenzake walipofikishwa mahakamani hapo kusikilizwa kesi yao inayowakabili.

Askari Polisi wakiwa na mbwa wao wakiimarisha ulinzi kwenye Mahakama ya Kisutu, wakati Sheikh Ponda na wenzake walipofikishwa Mahakamani hapo kusomewa mashtaka yao yanayowakabili.

Askari Polisi wakizunguka na mbwa kuweka usalama maeneo ya Mahakama ya Kisutu walikofikishwa Sheikh Ponda na wenzake.
Askari wa kikosi cha Farasi wakizunguka hapa na pale kuangalia usalama maeneo ya Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam leo.
Askari wa Kikosi cha Farasi wakiranda randa katika kuweka amani maeneo ya Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo, walipofikishwa mahakamani hapo Sheikh Ponda na wenzake.
Magari ya Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU), yakitoka kumsindikiza Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake .
Baadhi ya watu wakikaguliwa kabla ya kuingia katika Mahakama ya Kisutu leo.
 
Askari Polisi akiwaelekeza Waislamu waliofika Mahakamani hapo kusikiliza kesi za ndugu zao.
 Askari akiwahoji wananchi waliotaka kuingia kwenye Mahakama hiyo leo, kufuatilia kesi za ndugu zao.
Magari ya Polisi wa Kikosi Maalum cha kuzuiya Ghasia yakitoka nje ya Mahakama kwa ajili ya kuweka usalama katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment