TANGAZO


Monday, November 5, 2012

Mabingwa wa mbio za mitumbwi za Balimi wapatikana


Mabingwa wa Mashindano ya Mitumbwi ya Balimi Mkoa wa Mwanza, timu ya Cheka na Wengi kutoka Misungwi, wakiwasili ufukweni baada ya kuongoza mbio hizo, zilizofanyika Mwaloni mkoani humo juzi.

Nahodha wa timu iliyoshinda ya wanaume kutoka Misungwi, Daniel Mugeng'a, akionesha kitita cha shilingi laki tisa baada ya kukabidhiwa juzi.
 
Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race), mkoani Mwanza upande wa wanawake, timu ya Wanawake na Maendeleo kutoka Misungwi, wakiwa hawaamini macho yao kama wameweza kushinda kwa kuwaacha mbali wenzao na kuwa mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa jumla ya shilingi laki saba (700,000), kama zawadi ya ushindi wa kwanza.
 
Wapiga makasia wakinyanyua makasia yao juu kabla ya kuanza kwa fainali za mashindano ya mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race), yaliyofanyika jijini Mwanza juzi.
 
Baadhi ya wapiga makasia wakinyanyua makasia yao juu kabla ya kuanza kwa fainali za mashindano ya mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race), yaliyofanyika jijini Mwanza juzi.
Mabingwa wa ngoma za asili wa mashindano ya ngoma ya Kanda ya Ziwa, kikundi cha Bujora wakitumbuiza mashabiki wa mashindano ya mitumbwi, yaliyofanyika kwenye fukwe za Mwaloni mkoani Mwanza, ambapo washindi watakaowakilisha mkoa huo, kwenye fainali wamepatikana.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butala (kushoto), akiteta jambo na Afisa Utamaduni na Michezo wa Manispaa ya Ilemela, wakati wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race), yaliyofanyika mkoani Mwanza juzi.

Msanii wa kikundi cha ngoma cha Bujora, akicheza na nyoka kwa kuingiza kichwa chake mdomoni wakati kikitumbuiza wananchi waliofika kushuhudia mashindano ya mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race), yaliyofanyika Mwaloni mkoani Mwanza juzi.
 
Nahodha wa timu ya Wanawake na Maendeleo ya Misungwi, Tabu Daudi, ambao ndio washindi wa kwanza kwa upande wa wanawake Mkoa wa Mwanza, akipokea zawadi yao ya ushindi wa kwanza wa mashindano ya mitubwi ya Balimi. Nahodha huyo, alikabidhiwa kitita cha shilingi laki saba (700,000).
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  Fimbo Butallah, akimuelekeza jambo Nahodha wa timu ya Wanawake na Maendeleo ya Misungwi, Tabu Daudi, ambao ndio washindi wa kwanza kwa upande wa wanawake Mkoa wa Mwanza mara baada ya kukabidhiwa zawadi yao ya ushindi wa kwanza kitita cha shilingi laki saba (700,000).
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria mashindano hayo, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka katika mashindano hayo. (Na Mpiga Picha Wetu)

No comments:

Post a Comment