TANGAZO


Thursday, November 1, 2012

Ajali nyingine ni za kujitakia angalia habari hii kutoka maeneo ya Mwanza

 


Pamoja na ujenzi mzuri wa kituo hiki cha abiria wavukao kutoka Sengereama kwenda Mwanza mjini kwenye Ziwa Victoria, lakini suala la usalama hapa ni ziro kabisa, magari hayo pichani yakisubiria kivuko lakini hakuna kizuizi chochote kinachozuia hata kwa dharura kama ikitokea bahati mbayha gari moja kugonga mwenzake. Lakini hata hivyo hakuna sababu yoyote ya magari haya kusubiri kivuko kwenye eneo hili la karibu na maji wakati eneo la kutosha lipo.
Magari yakiwa kwenye foleni ya kuingia kwenye Kivuko cha Mv Misungwi, umbali wa kuvuka kwenye eneo hili nitofauti na ule umbali wa Kigamboni na Posta ambao huchukua dakika tano , hapa ni mwendo wa dakika 20 kufika ng'ambo ya pili.
Tatizo la kuondoa Kivuko kabla ya watu hawajaisha kuingia nalo hujitokeza maeneo mengi ya vivuko, sababu haijulikani, pichani kushoto, mfanyakazi wa kivuko akiondoa kamba iliyofungiwa kivuko kabla ya watu hawajaisha kuingia na kivuko kimeanza kutoka na kuwafanya abiria hao kukimbilia kwa kasi ili kukiwahi kivuko, huku wengine wakiwa na watoto wadogo.
 
Kiwango cha ubebaji wa mizigo ni cha kutosha kwa kivuko hiki kulingana na idadi ya watu waliopo, hata hivyo kuna vivuko viwili ambavyo hupishana kwa zamu.
Muonekano (mandhari) wa eneo la kandokando ya Ziwa Victoria.

No comments:

Post a Comment