Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa (kulia), akifafanunua masuala mbalimbali ya uchumi katika mkutano wa IMF nchini Japan, jijini Tokyo. (Picha zote na Ingiahedi Mduma, Scola Malinga, Tokyo- Japan)
Mkurugenzi Mtendaji anayeiwakilisha Afrika katika Shirika la Fedha, Bw. Moeketsi Majoro akiwa na ujumbe wake katika mkutano wa IMF, jijini Tokyo, nchini Japan.
Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akiwa na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha Bi. Monica Mwamunyange na Bi. Mwanaidi Mtanda Mhasibu Mkuu wa Serikali katika mkutano na Mkurungenzi Mtendaji anayewakilisha Afrika katika Shirika la Fedha la Kimataifa, Bw. Moeketsi Majoro, jijini Tokyo, nchini Japan.
Mhe. Mgimwa na Mkurungenzi Mtedaji anayeiwakilisha Afrika IMF, akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu Bw. S. Likwilile kwenye mkutano wa IMF, jijini Tokyo, nchini Japan.
Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akiwa na ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa IFM, jijini Tokyo, nchini Japan.
Na Ingiahedi Mduma, Tokyo – Japan
08 Oktoba, 2012
WAZIRI wa Fedha, Dk. William Mgimwa amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa kundi namba moja la Kanda ya Afrika anayewakilisha nchi za Afrika kwenye Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Moeketsi Majoro.
Hivi karibuni Rais Jakaya Mrisho Kikwete alimteua Dk. William Mgimwa kuwa Waziri wa Fedha nchini Tanzania ikiwa ni mara ya kwanza akiwa kama Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki ya Dunia kuhudhuria Mikutano hii ya Benki ya Dunia na Shirika la fedha la kimataifa inayofanyika hapa nchini Tokyo-Japan. Akiwa katika Mikutano hiyo, Mgimwa amefanikiwa kuonana na Bw. Moeketsi na kufanya mazungumzo mbalimbali naye, mojawapo likiwa ni jinsi gani Tanzania inaweza kufaidika na IMF na kuweza kuinua uchumi wake kupitia shirika hilo.
Akizungumza na Bw. Moeketsi, Wairi Mgimwa alisema, "Nina mambo muhimu manne ambayo ukisaidia kufikisha ujumbe huu na kama tutafanikiwa kupata fedha hizo, tutakuwa tumepiga hatua sana katika kuinua uchumi wa nchi yetu. Mojawapo ni kurekebisha barabara zetu na kuziweka katika viwango vinavyotakiwa, pili ni mfumuko wa bei, kwakweli mfumuko wa bei umekuwa ukisababishwa na upandaji wa bei za bidhaa hasa vyakula kama vile mahindi lakini tumegundua kuwa mchele unapanda sana hata kuzidi mahindi, tatu ni hii hali ya Tanesco, kwa kweli umeme umekuwa ni tatizo kwetu pamoja na jitihada zote tunazozifanya na hasa za kutumia gesi.”alieleza Mgimwa.
Aliendelea kusema kuwa tunahitaji kuimarisha masoko ya ndani na kuwa na dhamana za kutosha, pamoja na kuwa tumeandaa mipango kamambe ambayo itatusaidia katika kutekeleza haya lakini bado tunahitaji nguvu kutoka shirika la fedha la kimataifa”.Naye Bw. Moeketsi alifurahishwa na uelewa wa Mhe. Mgimwa na kumhaidi kufuatilia kwa karibu, kwani mambo yote aliyoyaeleza ni ya msingi na kwa sababu yako kwenye mpango mzuri yataweza kutekelezeka. Mazungumzo ya Mhe. Mgimwa na Bw. Moeketsi yamefungua mianya mipya na mahusiano ya karibu kati ya na shirika la Fedha la kimataifa na nchi ya Tanzania.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Benno Ndulu, Kamishna wa fedha za nje, Bw. Said Magonya, Bi. Mwanaidi Mtanda ambaye ni Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bw. Beda Shallanda ambaye ni Kamishna wa sera, Bi. Monica Mwamunyanye ambaye ni Kamishna wa Bajeti, Bw. Ahmed Rutashobola ambaye ni mwakilishi wa Tanzania huko IMF na baadhi ya maafisa kutoka Benki kuu na Wizara ya Fedha .
Aidha Mhe. Mgimwa, alimalizia kwa kueleza kuwa Tanzania imejitahidi sana kupunguza deni la Taifa na vilevile inafanya jitihada za kuimarisha usimamiaji wa deni hilo kwa kuhamishia jukumu hilo Wizara ya Fedha ili kuweka usimamizi na udhibiti wa karibu zaidi.
Nchi za Afrika zimegawanywa katika makundi matatu na Bw. Moeketsi anaziwakilisha nchi ishirini na moja za Afrika ambazo ziko kwenye kundi la kwanza.
No comments:
Post a Comment