TANGAZO


Monday, October 8, 2012

Ikulu yatwaa makombe mashindano ya SHIMIWI Morogoro


Mgeni rasmi, Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Peter Ilomo, akikagua timu ya Ikulu Sports Club, timu  ya kamba wanaume, aliyemwakilisha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kwenye kilele cha mashindano ya Shimiwi mkoani Morogoro juzi Jumamosi, Oktoba 6.10 2012.
Wachezaji wa timu ya Netball ya Ikulu Sports Club, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wao kabla ya fainali na timu ya Wizara ya Afya. Katika mchezo huo, Ikulu Sports Club ilishida kwa magoli 50 - 25 na hivyo kuwa washindi wa kwanza.
Wachezaji wa Ikulu Sports Club na Wafanyakazi wenzao, ambao walienda kushangilia timu yao, wakifurahia baada ya kushinda na kupata vikombe vitano kwenye michezo ya mpira wa pete, kamba wanaume, kamba wanawake, kuendesha baiskeli na ushindi wa pili wa riadha.
Ikulu Sports Club, wavuta kamba wanaume, wakifurahia kikombe baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi, Katibu Mkuu, Ikulu Bw. Peter Ilomo.
Wachezaji wa Ikulu Sports Club wakiwa na vikombe vyao walivyovitwaa baada ya kuongoza kwa kupata vikombe vitano kwenye mashindano ya Wizara na Taasisi za Serikali (SHIMIWI), mashidano yalifanyika mkoani Morogoro na kufungwa na Katibu Mkuu, Ikulu Bw. Peter Ilomo.

No comments:

Post a Comment