TANGAZO


Monday, October 8, 2012

Watu wawili wafariki katika ajali iliyohusisha bodaboda na gari dogo la Toyota Starlet, Makongo jijini Dar es Salaam

Dereva wa Bodaboda na abiria wake, ambao hawakuweza kufahamika majina yao mara moja, wakiwa wamelazwa pembeni mwa barabara ya Bagamoyo eneo la Makongo, baada ya kugongwa na gari aina ya Starlet yenye namba za usajiri T 838 BKB, wakati wakiwa kwenye pikipiki yao, yenye namba za usajili  T491 BFY na kufariki dunia papo hapo. Ajali hiyo imetokea leo asubuhi. Pichani ni mwananchi, akijaribu kuutambua mmoja wa mwili wa marehemu hao katika ajali hiyo. 

Mwananchi akijaribu kutambua moja ya mwili wa marehemu waliofariki katika ajali hiyo ya gari la bodaboda. 

Wananchi waliofika katika tukio hilo, wakiangalia ajali pamoja na maiti zilizofunikwa, zikiwa zimelazwa pembeni mwa gari lililogongana na bodaboda waliokuwa wamepanda marehemu hao, ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja. (Picha zote na sufianimafoto)

No comments:

Post a Comment