Mmoja wa wanawake walionufaika na mradi wa kuwawezesha wanawake
wanaonyonyesha na wajawazito mkoani Mtwara, kupata chakula chenye lishe
akiijaribu simu aliyopatiwa ikiwa na fedha katika akaunti ya M-pesa,
atakazozitumia kununulia chakula chenye lishe. Fedha na simu hizo
hutolewa bila malipo na Shirika la
Mpango wa Chakula Duniani – WFP, kupitia mradi wake wa Lishe bora na salama.
Mmoja wa
wanufaika wa mradi wa kuwawezesha wanawake wanaonyonyesha na wajawazito mkoani Mtwara kupata chakula chenye lishe, akiijaribu simu aliyopatiwa ikiwa na fedha katika
akaunti ya M-pesa, atakazozitumia kununulia chakula chenye lishe. Fedha na simu
hizo hutolewa bila malipo na Shirika la
Mpango wa
Chakula Duniani – WFP, kupitia mradi wake wa Lishe bora na salama.
Ofisa Elimu, Wilaya ya Mtwara,
Mwalimu Mohamed Kahumbi, akionesha aina ya
simu iliyowekewa fedha katika akaunti ya M-pesa zinazotolewa bila malipo kwa akina mama wanaonyonyesha
kuwawezesha kupokea fedha za kununulia chakula chenye lishe kupitia mradi wa Lishe bora na salama wa shirika la mpango wa chakula
duniani – WFP. Mradi
huo umezinduliwa juzi katika kijiji cha Nanguruwe, Mkoani
Mtwara.
Afisa Elimu Wilaya ya
Mtwara Mwl.Mohamed Kahumbi akimkabidhi simu ya mkononi mmoja
wa wanufaika wa mradi wa Shirika la
Mpango wa Chakula Duniani – WFP wa kuwapatia fedha wanawake wanaonyonyesha na
wajawazito fedha za kununulia chakula chenye lishe kupitia M-pesa wakati wa uzinduzi uliofanyika juzi katika kijiji cah Nanguruwe mkoani
Mtwara.
Akina mama wa kijiji cha
Nanguruwe, mkaoni Mtwara ambao ni wanufaika wa mradi wa Shirika la Mpango wa
Chakula Duniani – WFP wa kuwapatia fedha
wanawake wanaonyonyesha na wajawazito za kununulia chakula chenye lishe wakijumuika na Maofisa wa Vodacom
kufurahia simu walizopatiwa zikiwa zimeunganishwa na mtandao wa Vodacom
kuwawezesha kupokea fedha za mradi kwa njia ya M-pesa.
No comments:
Post a Comment