Moja ya Picha iliyotoka kwenye magazeti: Baadhi ya askari wakionekana kumsulubu Mwangosi huku nyuma kushoto mmoja wao akionekana kumfyatulia bomu la kutoa machozi kwa karibu kabisa |
RIPOTI YA TIMU
MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA
WAHARIRI TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA KWA MWANDISHI
WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012 KATIKA KIJIJI CHA NYOLOLO, WILAYA YA
MUFINDI, MKOANI IRINGA
Ripoti ya Timu
Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Hadidu za Rejea Timu hiyo ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania
Septemba 5, 2012.
Imewasilishwa
na:
John P. Mireny -
Kiongozi wa Timu, MCT
Hawra Shamte -
Mhariri wa Siasa, Gazeti la Mwananchi, TEF
Simon S. Berege
- Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu Tumaini, Iringa
ORODHA YA
UFUPISHO
CHADEMA – Chama
cha DemokrasianaMaendeleo
CPJ – Kamati ya
Kutetea Waandishi wa Habari
DCI - Mkurugenzi
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
IPC - Klabu ya
Waandishi ya Iringa
M4C - Harakati
za Mabadiliko
MISA - Taasisi
ya Vyombo vya Habari ya Kusini mwa Afrika
OC-CID - Mkuu wa
Uchunguzi wa Makosa ya Uhalifu wa Wilaya
OCD - Mkuu wa
Polisi Polisi wa Wilaya
RPC - Mkuu wa
Polisi wa Mkoa
TEF - Jukwaa la
Wahariri Tanzania
UNESCO - Shirika
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni Ripoti ya Timu Maalum ya
Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu
za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
1.0 Muhtasari wa
ripoti
Ripoti hii ni ya
wa uchunguzi mazingira yaliyopelekea kuuawa kwa Mwandishi wa Channel Ten Daudi
Mwangosi mikononi mwa polisi katika kijiji cha Nyololo, wilaya ya Mufindi, Mkoa
wa Iringa Septemba 2, 2012.
Baraza la Habari
Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa pamoja waliunda timu ya
uhunguzi. Mchakato wenyewe ulihusisha mbinu za uchunguzi za kiuandishi wa
habari
ambazo si kama
za uchunguzi wa kipolisi na wa kimahakama.
Methodolojia za
uchunguzi zilijumuisha mahojiano, kutembelea maeneo husika na uchambuzi mahsusi
wa nyaraka kwa kuzingatia adidu za rejea zilizopo. Waandishi wa Habari
waliokuwepo Nyololo na ambao hawakuwepo katika eneo la mauaji wametoa mchango
muhimu.
Mashahidi
walioshuhudia katika kijiji cha Nyololo, wakiwemo watoto walikuwa vyanzo Muhimu.
Habari zilizochapishwa katika vyombo vya habari kutokana taarifa rasmi kuhusu
baa hilo pia zilichambuliwa kwa umakini.
Uchambuzi mpana
ulifanywa kuhusu hali ya mahusiano ya Uongozi wa Mkoa wa Iringa ( ikiwemo
polisi) na wanahabari wa Iringa kabla ya mauaji ya Mwangosi.Mahusiano yalikuwa
si mazuri na ya shaka kati ya pande hizo mbili tangu katika robo ya mwisho ya
mwaka 2011.
Hii ilisaidia
kupata picha pana ya tatizo pamoja na kuweza kufahamu kwa undani tatizo lenyewe
na kuweza kupanga mwelekeo wa uchunguzi wenyewe na hatimaye kuwezesha timu
kuweza kuunganisha mambo na kuandaa ripoti hii.
Aina nyingine ya
ushahidi uliosaidia kuimarisha ripoti hii ni pamoja na video, picha mgando;
maelezo kutoka katika mikutano na waandishi wa habari iliyofanyika Iringa na
taarifa za vyombo vya habari.
Mpaka wakati
ripoti hii inaandikwa, taarifa rasmi kuhusu mauaji ya David Mwangosi zimekuwa
zikitofautiana.
Kwa kifupi
matokeo ya mambo yaliyopelekea mauaji ya Daudi Mwangosi kwanza Yanadhihirisha bila wasiwasi kwamba Polisi kwa
makusudi waliwaburuta waandishi waliotoka Iringa waliokuwa wakifuatlia habari za
shughuli za Chadema katika kijiji cha Nyololo. Zaidi ya hapo, Daudi Mwangosi
mwenyewe aliuliwa akiwa mikononi mwa polisi huku wakiangaliwa na Kamanda wa
Polisi wa Mkoa, Michael Kamuhanda.
Uamuzi huu
unadhihirishwa na ushahidi uliokusanywa kwenye maeneo pamoja na video na taarifa
zingine za vyombo vya habari.
2.0 Tamko la
Tatizo
Kuanzia Machi
2012 mahusiano ya kikazi kati ya waandishi wa habari wa mkoa Iringa na viongozi
wa utawala wa mkoa, ikiwemo jeshi la polisi, haukuwa mzuri.
Katika mikutano
yake mbalimbali ya kitaaluma, Klabu ya Waandishi Habari ya Iringa (IPC) kutoka
katika robo ya mwisho mwaka 2011, waandishi wa habari wamekuwa wakilalamikia
“kutotendewa sawa” na maofisa wanapokuwa wakifuatilia na kuandika habari mkoani
Iringa.
Kwa mfano ,
Novemba 2011, mwandishi Laurean Mkumbata anayeandikia ITV alipigwa vibaya na
kamera yake ikaharibiwa na aliyekuwa mkuu wa polisi (OCD) wa wilaya ya Iringa ,
wakati mwandishi huyo alipokuwa kazini.
Mkumbata
alieleza mbele ya Timu ya Uchunguzi kwamba yeye na waandishi wengine akiwemo
marehemu Daudi Mwangosi walikuwa wakikusanya habari katika mpambano kati ya
polisi na kundi moja la watu mjini Iringa. Kundi hilo lilitaka kuchoma moto
nyumba moja iliyodaiwa kuwa na wachawi ambao uwepo wao ulikuwa ukiathiri eneo
lote jirani.
Hali
iliyojitokeza ni kwamba ofisa yule wa polisi alitaka kuharibu kifaa cha kazi cha
mwandishi ili kuzuia upelekaji wa habari kuhusu mpambano wa wananchi wenye
hasira na polisi.
Wakati polisi
walikuwa wakiwadhibiti watu hao kwa kutumia mabomu ya machozi na kufyatua risasi
za moto hewani kuwatisha na kuwaondoa watu hao kutoka eneo la tukio, OCD Semunyu
alimshika mwandishi huyo na kumnyang’anya kamera yake ambayo aliipiga chini mara
tatu, na hivyo kuiharibu kabisa.
Pamoja na hayo,
Mkumbata alishikiliwa kwa muda alipokwenda kutoa taarifa kuhusu tukio hilo
katika makao ya polisi ya mkoa. Baada ya hapo jitihada za kuficha ukweli
zikaanza.
Hata hivyo,
aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa (RPC), Evarist Mangala aliingilia
kati na kumwamuru ofisa aliyehusika, Semunyu, kulipa kamera iliyovunjwa. Ofisa
huyo alitekeleza amri hiyo na Mkumbata alipata kamera yake. Ofisa huyo alilipa
kutoka mfukoni mwake.
Mkumbata
anaamini kwamba ofisa yule wa polisi aliipiga chini kamera yake mara tatu
kuhakikisha inaharibika kabisa na hakuna kinachopatikana, hatua iliyolenga
kuhakikisha mwandishi huyo hawezi kutangaza taarifa za tukio kwa
wakati.
Tangu wakati huo
hali ya kutiliana shaka imekua katika mahusiano ya wanahabari wa Iringa na
Polisi. Mahusiano na viongozi wengine wa mkoa nayo hayajakuwa mazuri tangu
kipindi hicho cha robo ya mwisho ya 2011.
Frank Leonard,
Katibu wa IPC anakumbuka kuwa mwishoni mwa Februari 2012, waandishi saba
waliteuliwa na IPC kuandika habari ya ziara ya Makamu wa Rais mkoani Iringa,
lakini walilazimika kulala ndani ya gari walilosafiria kwa kuwa maofisa wahusika
wa mkoa walidaiwa kupuuza kuwapatia hoteli ya kulala.
Tukio hilo
liliudhi uongozi wa IPC ambao uliandaa maandamano ya amani kulalamikia unyanyasi
wa waaandishi wa habari unofanywa na viongozi wa mkoa.
Hatua hiyo, kwa
mujibu wa Katibu huyo ililenga kuwasilisha kwa viongozi wa mkoa msimamo kwamba
“Wanachama wa IPC hawaegemei chama chochote cha siasa, bali ni wanataaluma na
wanaosimamia uandishi habari unaozingatia maslahi ya umma”.
Machi 6, 2012,
mamlaka ya polisi ya mkoa uliidhinisha ombi la IPC kuandamana kupinga kuendelea
mahusiano yasiyo mazuri kati ya waandishi wa habari na uongozi wa
mkoa.
Katibu wa IPC
anakiri kwamba mahusiano kati ya pande hizo mbili yaliboreka baada ya maandamano
hayo ambapo aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa aliahidi kushughulikia tofauti
zilizopo na kuhakikisha kunakuwa na maelewano.
Kubadilika kwa
mambo ghafla na kufikia mauaji ya Daudi Mwangosi hapo Septemba 2, 2012, wakati a
akikusanya habari za shughuli za kisiasa za Chadema katika wilaya ya Mufindi ,
katika kijiji cha Nyololo mikononi mwa polisi wanaotuhumiwa kwa mauaji inastusha
na ni jambo lisilo la kutegemewa kwa Frank Leaonard.Marehemu Daudi Mwangosi
alikuwa Mwenyekiti wa IPC.
3.0
Mamlaka
Mamlaka ya
uchunguzi huu inatokana na katiba ya Baraza la Habari Tanzania (MCT), kifungu 3
(e), kinachoelezea malengo ya Baraza kuwa ni:
Kuwa na rejista
ya matukio yanayoweza kukwaza upatikananji wa habari za manufaa kwa umma na
muhimu, na kuchunguza tabia za watu, mashirika na vyombo vya serikali kwa ngazi
zote dhidi ya vyombo vya habari, na kutangaza matokeo ya uchunguzi
huo.
3.1
Lengo
Lengo la
uchunguzi huo ni kuweka rekodi sawa ya mazingira yaliyopelekea kuuawa kwa
mwandishi wa Channel Ten na Mwenyekiti wa IPC, David Mwangosi , Septemba 2, 2012
katika kijiji cha Nyololo , wilaya ya Mufindi, mkoa wa Iringa .
Uchunguzi huo ni
huru na sio kama wa kipolisi au wa kimahakama lakini ni jitihada za dhati za
kuweka kumbumbuku ya hali ya mambo kuhusu kifo cha kwanza cha mwandishi wa
Tanzania akiwa kazini.
4.0 Adidu za
Rejea
Timu ya
uchunguzi iliongozwa na Adidu za Rejea zifuatazo:
4.1 Lengo
Kuu
Kuchunguza hali
iliyopelekea kuuawa kwa David Mwangosi.
4.2 Malengo
mahsusi
Kuchunguza
chanzo cha kuwepo uhusiano usio mzuri kati ya IPC na uongozi wa kiutawala wa
Iringa .
Kuwahoji
wanakijiji wa Nyololo kuhusu hali halisi iliyosababisha mapambano kati ya
polisi/ Chadema/ waandishi wa habari.
Kukusanya
maelezo stahili kutoka kwa wananchi, IPC na mashuhuda waandishi waliokuwepo
kwenye eneo la ghasia.
Kuchambua kwa
uhuru ripoti za vyombo vya habari, ripoti rasmi na za polisi na madai kuhusu
tukio hilo.
5.0 Muda wa
kukamilisha jukumu
Kazi hiyo
ilichukua siku nane (8) kuanzia Septemba 5, 2012 na kumalizika Septemba 12,
2012.
6.0
Methodolojia
Timu ilianza
uchunguzi kama ifuatavyo:
Kwanza kabisa,
hati na taarifa za magazeti kuhusiana na uchunguzi huo zilipitiwa ili kupata
msingi wa suala hilo. Hii inajumuisha mamlaka ya kikatiba ya MCT kufanya
uchunguzi kama huo.
Pili, Timu hiyo
imechunguza kwa karibu jinsi vyombo vya habari vilivyotangaza zikiwemo picha
mgando, na video kuhusu kuuawa kwa Daudi Mwangosi hapo Septemba 2, 2012, na
taarifa za awali za polisi dhidi ya mambo yaliyogunduliwa na wachunguzi katika
uchunguzi wao.
Taarifa zote
zilizoripotiwa na polisi na Waziri mwenye dhamana kuhusu mauaji ya mwandishi
kabla yataarifa ya kuundwa kwa kamati maalum ya uchunguzi ya Waziri wa Mambo ya
Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi Septemba 4, 2012 yanachambuliwa kwa kina.
Hatimaye,
uchunguzi katika eneo. Hii ilihusisha kusafiri kwenda Iringa na kufanya
mahojiano na watu walioteuliwa na wanahabari katika kijiji cha Nyololo
waliokuwepo siku Mwangosi. Utaratibu wa mahojiano ya mtiririko kutokana na
majibu ulitumiwa na wachunguzi kwa watu
mbalimbali.
Utaratibu mkuu
ulikuwa ni mazungumzo ya bayana kati ya wachunguzi na watu mbalimbali wakiwemo
baadhi ya wanakijiji wa Nyololo. Mbinu za kiuchunguzi za uandishi wa habari
zilitumika kufanikisha lengo la jukumu hilo.Matokeo yake, mchakato huo
uliwezesha kupatikana ukweli uliowezesha kukamilisha ripoti.
7.0
Matokeo
7.1 Maelezo ya
awali
Hapo Septemba 2,
2012, mikutano miwili tofauti ya waandishi wa habari iliyosheheni ilifanyika
katika Manispaa ya Iringa kwa nyakati tofauti siku hiyo. Mkutano wa kwanza
uliitishwa na kuhutubiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa (RPC), Michael
Kamuhanda katika ofisi yake asubuhi.
Mada ya mkutano
huo ni uamuzi wa polisi kuzuia mikutano ya kisiasa iliyopangwa na chama cha
upinzani cha Chadema katika mkoa wa Iringa iliyolenga kutelekeza kampeni za
chama hicho za Kuleta Mabadiliko nchi nzima.
Kamanda wa
Polisi wa Mkoa alitahadharisha kuwa sensa ya watu na makazi ambayo awali ilikuwa
ilipangwa kufanyika Agosti 26 – Septemba 1, 2012, imeongezewa muda na serikali
hadi Septemba 8, 2012, na mikusanyiko ya kijamii na mikutano ya kisiasa
imesimamisha mpaka zoezi hilo likamilike.
Waandishi wa
habari waliokuwepo kwenye mkutano huo wanakiri kwamba katika mkutano huo
marehemu Daudi Mwangosi alikuwa ni ripota pekee aliyemuuliza RPC “maswali
magumu” kiasi cha kumkera kiongozi huyo wa polisi.
Mojawapo ya
maswali yaliyoulizwa na Mwangosi ni ufafanuzi sahihi wa nini hasa ni “ mkutano
wa ndani wa chama” kulingana na madai ya maofisa wa Chadema kwamba chama hicho
hakipangi kufanya mikutano ya hadhara na maandamano ya kisiasa bali ni kufungua
matawi mkoani Iringa bila kufanya mikutano.
Katibu wa IPC
anakumbuka swali moja la Mwangosi kwenye mkutano huo ambalo lilimuudhi RPC.
Aliuliza: kwanini chama tawala cha CCM kiko huru kufanya mikutano ya kisiasa
wakati chama cha upinzani kama Chadema kinawekewa vikwazo na polisi kila
wakati.
Wakati marehemu
Mwangosi akisisitiza ufafanuzi zaidi kutoka kwa Mkuu huyo wa polisi wa mkoa, RPC
alisisitiza : “ Hii ni amri na polisi hairuhusu maswali zaidi kuhusu suala
hili”.
Na taarifa
kutoka kwa RPC imewakumbusha wazi wanasisasa, vyama vya siasa na wananchi kwa
jumla kwamba “mikutano ya vyama vya kisiasa imezuiliwa kutokana na kuendelea kwa
sensa ya watu na makazi kwa siku saba zaidi kuanzia Septemba 2,
2012.
Mara baada ya
mkutano na RPC baadhi ya maofisa wa polisi walionyesha kuwa mambo hayatakuwa
sawa katika kijiji cha Nyololo village Waandishi wengine wa Iringa, Clement
Sanga anayeandikia magazeti ya Mwananchi Communications Ltd na Oliver Motto,
mwandishi wa
kujitegemea wa
gazeti la Mtanzania, Star TV na Radio Free Africa walisema haya :
“Baada ya
mkutano huo na waandishi , wakati wanahabari wakitoka kwenye ofisi za mkoa za
Polisi, baadhi ya polisi walisikika bila wao kuwa wakiwaonya wasiende Nyololo
kwa ajili ya kukusanya habari za shughuli za siasa za Chadema kutokana na kuwa
na uwezekano wa hatari”.
Mkutano wa pili
wa waandishi uliitishwa mchana na Chadema na ukahutubiwa na Katibu Mkuu na
Dk.Wilbroad Slaa na kamanda wa Kampeni ya Mabadiliko ya chama hicho Benson
Kigaila.
Katika mkutano
huo , Chadema ilichachamaa na kutetea kampeni zake za mabadiliko na kushutumu
polisi kwa kufanya njama za kuzima kamepni hizo. Chadema ilihoji kwanini polisi
inabagua vyama vya upinzani wakati wakipendelea chama tawala CCM kwa madai ya
kusimamia sheria.
Licha ya kuwepo
amri ya polisi ya kuzuia mikutano yote ya siasa mpaka zoezi la sensa ya watu na
makazi lililoongezewa muda limalizike , Chadema ilidai kwenye mkutano huo kwamba
kampeni za uchaguzi za CCM katika uchaguzi mdogo ziliruhusiwa kufanyika katika
jimbo la Bububu , Zanzibar.
Kampeni za
uchaguzi mdogo wa Bububu zilizinduliwa Jumapili Septemba 2, 2012 na Makamu wa
Rais wa serikali ya Muungano, Dk. Mohammed Gharib Bilal.
Hivyo kwa ufupi,
Chadema iliamua kuendelea na kampeni zake mkoani Iringa , ikiwemo kufungua
matawi ya chama katika kijiji cha Nyololo,
wilaya ya
Mufindi Jumapili Septemba 2, 2012, lakini bila kufanya mikutano ya hadhara.
Hatimaye maofisa walishikilia msimamo wao na kuendelea kufufungua matawi ya
chama Nyololo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa Iringa, RPC Michael Kamuhanda, alipanga
askari wake kwenye magari ya wazi kufuatilia msafara wa maofisa wa Chadema.
Pande hizo mbili zilikutana
kwenye kijiji
cha Nyololo.
Viongozi wa
Chadema walipanga kufungua matawi mawili katika kijiji cha Nyololo village,
kiasi cha kilomita 500 (315 maili) magharibi mwa Dar es Salaam, na mwendo wa saa
tatu kwa gari kutoka Manispaa ya Iringa.
Matawi hayo yako
umbali wa kilomita tatu kutoka kila moja yakitenganishwa na barabara kuu ya Dar
es Salaam -Tunduma.
Mchoro uliopo
ukurasa wa 16 unaonyesha hali halisi ilivyokuwa, kama ilivyoelezwa na mashuhuda
waliokuwepo na kuboreshwa na wachuguzi.
Kwa lengo la
kuonyesha , maeneo mawili yamewekewa alama tofauti ya A ikimaanisha “eneo
tulivu” na B ikimaanisha “eneo la umwagaji damu”.
Katika eneo la
[A], ambapo utulivu ulikuwepo na ulizingatiwa na polisi katika maamuzi na
matendo yao ambapo vurugu na umwagaji damu uliepukwa. Eneo lingine ni [B],
ambapo polisi ilitumia, nguvu zaidi na kupelekea mauaji ya Daudi Mwangosi na
kujeruhi waandishi wengine
kadhaa wa Iringa
na makada wa Chadema.
7.2 Eneo la
matukio ya utulivu [A]
Hapa ni sehemu
ya kwanza lilipo tawi la Chadema kusini mashariki mwa barabara ya changarawe
inayopita kijiji cha Nyololo, kutoka barabara kuu ya Dar-Tunduma. Mashuhuda
(waandishi na wanakijiji) wal;isema kuwa baada ua kuwasili kwenye eneo la tawi,
maofisa wa Chadema na wanachama walishuka kutoka kwenye magari wakiwa tayari
kuanza shughuli. Ukanda wa njano uliwekwa kuzunguka ofisi ya Chadema kuzuia watu
kukusanyika katika
jingo la ofisi
hiyo.
Mara baada ya
Chadema kuanza mkutano wao wa ndani kikundi cha askari wa kikosi cha kuzuia fufo
(FFU) kilifika eneo hilo na kujipanga kwa muundo wa kijeshi wa V. Kikosi hicho
kilikua chini ya uongozi wa Ofisa wa kudhibiti uhalifu wa mkoa (RCO) SSP Nyigesa
Wankyo.
Kamanda wa
kikundi cha FFU OC Florent Mnunka anaamuru polisi wainue bendera nyekundu yenye
maandishi ya kuwataka watu waliokusanyika kutawanyika ama vinginevyo watatumia
nguvu. Kamanda huyo anatangaza “Watu wote mliokusanyika hapa, mnaamriwa na
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania mtawanyike mara moja na kwa amani, vinginevyo
tutatumia
nguvu ” anarudia
maneno hayo . Baada ya kurudia amri hiyo mara tatu, OC-CID anaamuru polisi
kusogea karibu na ofisi ya Chadema.
Wakati
wakisogelea eneo hilo la Utulivu [A] , Kamanda wa kampeni ya mabadiliko ya
Chadema Benson Kigaila na viongozi wengine walitoka nje ya ofisi hiyo na
kumuomba kamanda wa FFU kuzuia askari wake kutumia nguvu bila sababu kwa kuwa
haikupanga kufanya mkutano wa hadhara wa kisiasa.
Viongozi wengine
waliokuwa na Kigaila walikuwa ni Alfred Lwakatare na Naibu Katubu Mkuu wa
Chadema Zanzibar , Said Issa Mohamed.
Pande hizo mbili
zilipingana kwa muda kuhusu maana sahihi ya“ mkutano wa ndani wa chama” na kama
maana yake ni tofauti na mikutano iliyozuiwa na polisi .
Ushahidi wa
picha za video uliopatikana na waandishi wa habari wengi unadhihirisha na
kuonyesha mvutano kati ya polisi na Chadema katika eneo tulivu[A] kama
ifuatavyo:
Benson Kigaila:
“ Sisi tuko katika ofisi ya tawi letu, tunajua sheria , hili ni
tawi la
Chadema”. Kamanda wa FFU : “Tunawaonyeni nyingi, tafadhali, fanyeni
mkutano
wenu ndani ya
ofisi” Benson Kigaila: “Hatuendi kokote ” Kamanda wa FFU: “Ingieni
ndani”
Ghafla RCO
akaingilia na kushauri viongozi wa Chadema kuwaambia wananchama wao waingie
ndani ya ofisi yao..Wanachama walikubali lakini wote wasingeweza kutosha kwa
sababu ofisi yenyewe ni ndogo. .
RCO akasisitiza:
“Huu ni mkutano usioruhusiwa, tafadhali ingieni ndani” Mwenyekiti wa Taifa wa
vijana wa Chadema (Bavita), John Heche akajibu : “Tatizo ni nini? Kama mmetumwa
kuua, fyatueni risasi na muue…sisi tutakaa hapa.”
Kijana mmoja wa
Chadema anasikika katika video akiwaambia polisi ; “Jana makada wa CCM
walirejesha fomu za uchaguzi wa chama chao kwa maandamano na sherehe … sisi
hatuko tayari kuondoka ”.
John Heche
anabishana na polisi akisema : “Mfahamu sheria zenu kabla ya kufanya kazi
yenu”
Mwishowe,
maelewano yalifikiwa kati ya RCO na maofisa wa Chadema ,na kamanda anaamuru
maofisa wake kutotumia nguvu dhidi ya watu waliokusanyika kwenye ofisi
ile.
Ofisa mmoja wa
Polisi analalamika , “Wanatupotezea muda wetu ….aaah wanachukua muda
wetu”.
Ofisa huyo
inaelekea alikuwa akilalamikia amri ya mwisho iliyotolewa na mkuu wake, RCO,
ikikitaka kikisi hicho kuacha kutumia nguvu, ikiwa inakiuka amri awa
awali.
Waandishi dhidi
ya RPC Kamuhanda Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Michael Kamuhanda anawasili kwenye
eneo la utulivu [A] dakika chake baada ya RCO, maofisa wa FFU na wa
Chadema kufikia
muafaka na kukubaliana kuhusu maana ya “mkutano wa ndani”.
Waandishi
waliokuwepo eneo hilo walimpokea kwa maswali kadhaa kuhusu tofauti za polisi na
Chadema. Marehemu Daudi Mwangosi akiwa mmoja wa waandishi hao waliomkabili
RPC.
Mwangosi
alimuuliza RPC: “Watu hawa wako katika eneo la ofisi yao, kuna tatizo lolote
linalotokana na shughuli wanazokusudia kufanya?”
RPC anamjibu
Mwangosi “Nimeshakuambia usiwe mbishi. Nilichokuambia ni kwamba nimezuia
mikutano yote ya kisiasa…Lakini usije na mambo yale yale asubuhi, jioni na
mchana, na jua linapozama…kuna umuhimu gani kutuuliza sisi tupo hapa kufanya
nini?”.
Mwandishi
mwingine (Jina lake halikutapitkana ) “Nafikiri wewe ndiye mbishi (RPC)” RPC
“Nilichozuia ni mikutano ya hadhara ya kisiasa, lakini shughuli zote za ndani
zinaruhusiwa kuendelea…hadi sasa hakuna tatizo”
RPC anaendelea:
“Tumefanikiwa kuzuia mikutano na ghasia… kama wanataka kufanya mikutano ya ndani
wanaweza kuendelea.” Mwangosi “…kama wanavyofanya sasa …..…”
RPC anajibu,
“Kama walivyofanya tangu juzi ”
Baada ya
kubadilishana maneno zaidi RPC anasema: “Tunawataka viongozi, hatutashughulika
na watu waliokusanyika hapa. Lengo letu ni kushughulikia walioitisha mkutano…
wao ndio chanzo cha kila kitu, na wanavunja amri rasmi”. Tunaogopa kuwajeruhi
watu bila sababu, hivyo
tutashughulika
na viongozi ambao ni kundi dogo na ni rahisi kulishughulikia” anasema RPC na
kuamuru “Sasa hakuna mkutano, huu (mkusanyiko) unaofanyika nje.”
Mwangosi
anaingilia: “ Huu ni mkutano ? RPC anaamuru mkusanyiko kuendelea na mkutano wao
ndani; “Ingia ndani” Mwandishi ( anayetambulika kwa kubeba kamera na akiwa
katika kundi la waandishi): “Inakuwaje kama chumba ni kidogo kutosha watu wote?”
RPC: “Tutawakamata ninyi viongozi kama mtaendelea ”Sauti ya mtu anayedhaniwa
kuwa kiongozi wa Chadema inasema: “Tutaendelea kuwapo hapa .”
RPC: “Ndiyo na
ninyi mko wachache, tunawamudu ” Mtu huyo anajibu : “Aah! Hamna tatizo… ni miaka
mingapi Mandela alikaa gerezani ”? RPC anajibu , “ Hata miaka 30, lakini
umemtaja Mandela, wewe Mandela?”
Wakati waandishi
wakimhoji RPC, maofisa wa Chadema waliendelea na mkutano wao na kuumaliza kwa
amani. Chadema walimaliza shughuli yao na wanahabari wakafanya kazi yao hapa
bila kunyanyaswa.
Baaada ya hapo
makada wa Chadema walipanda basi lao kwenda kaskazini magharibi kwenye ofisi
nyingine. Katika eneo hili la utulivu. [A],mabomu ya machozi hayakulipuliwa wala
risasi hazikupigwa kuwatisha watu. Pia hakuna mtu aliyeuawa.
7.3 Eneo la
umwagaji damu [B]
Mara baada ya
maofisa wa Chadema kumaliza ufunguzi wa tawi katika eneo la utulivu [A],
walikwenda kukamilisha shughuli katika eneo la umwagaji damu [B].
Inachukua chini
ya dakika 20 kutembea kufika katika ofisi ya pili ya Chadema. wakati maofisa wa
chama wakielekea katika eneo hilo, polisi waliwafuata kwa karibu. Waandishi wa
habari pia waliwafuatilia ili kukusanya habari za shughuli hiyo.
Lakini kitu
kimoja kibaya kilitokea hata kabla ya askari wote wa FFU kufika katika eneo la
Umwagaji damu [B].
Mashuhuda
wanaeleza kuwa RPC alimwita RCO na kumuonya wazi kuhusu “ kushughulikia kwa
amani’ masuala ya Chadema katika eneo la awali la utulivu [A].
Inaelekea RCO
alijitoa kuelekea eneo la umwagaji damu [B], na hivyo usimamizi wa utoaji
maamuzi katika Eneo la Umwagaji damu [B] ulibakia kwa mkuu wake ambaye ni RPC
Michael Kamuhanda.
Mabishano na
waandishi wa habari kama yaliyotokea katika eneo la la awali yaliibuka
tena.
Hapa makada wa
Chadema walikusanyika nje ya ofisi yao wakiimba t“Wamezoea kuua , wamezoea
kuua”. Inaelekea wimbo huo uliwaudhi polisi.
Vurugu zikaanza
pale RPC alipoamuru kukamatwa kwa viongozi wa Chadema waliokuwepo, kwa mujibu wa
watu walioshughudia. Kufuataia amri hiyo ya RPC kulingana na mashuhuda , polisi
kwanza waliingia kwa nguvu katika ofisi ya Chadema, wakipiga mabomu ya machozi
na
kuaamuru
viongozi hao wajisalimishe.
Baada ya polisi
kutumia nguvu, kiongozi wa kampenu za mabadiliko wa Chadema mkoani Iringa,
Benson Kigaila , aliwaomba wafuasi wachache wa chama hicho na viongozi
waliokuwepo kujisalimisha kwa kuketi na kuinua mikono yao juu”.
Waandishi wawili
waliohojiwa, Clement Sanga wa Mwananchi Communications Ltd na Oliver Motto,
mwandishi wa kujitegemea wa Mtanzania, Star TV na Radio Free Africa walishuhudia
ghasia hizo katika kijiji cha Nyololo village, wakati wakiwa wamekimbilia sehemu
ya
barabarani,
hatua chache kutoka eneo hilo la umwagaji damu B.
Waandishi hao
walisema kuwa wakati makada wa Chadema walitii maagizo ya viongozi wao ya kuketi
na kuinua mikono yao juu, polisi walifyatua risasi na n a mabomu ya machozi, na
kuwapiga makada hao na waandishi kwa virungu.
7.4 Matukio
yasiyo ya kawaida katika Eneo la Umwagaji Damu (B)
Jambo moja la
kushangaza katika eneo la umwagaji damu B ni kuwepo kwa raia wachache (makada wa
Chadema na waandishi kwa pamoja), wakiwa wamezidiwa kabisa na idadi ya polisi.
Maelezo ya mashuhuda, picha mgando na video zinadhihirisha hii bila shaka
yoyote.
Wanakijiji wa
Nyololo waliohojiwa walisema kwamba Jumamosi Septemba 1, 2012 watu wanaoaminika
kuwa ni askari kanzu walifika eneo hilo na kuwaonya wakazi wake kuhusu ya hatari
inayowza kutokea kama wakihudhuria shughuli za ufgunguzi wa matawi ya Chadema.
Walidai kuwa
walishauriwa pia kuondoka katika maeneo yao wakati wa saa za mchana Jumapili
Septemba 2, 2012 wakati ambao Chadema imepanga kuendesha shughuli
zake.
Mkakati wa
kutisha ulifanikiwa kwa sababu watu wazima wakazi wa Nyololo waliohojiwa baadaye
walisema hawajui kuhusu vurugu za polisi na Chadema kwa sababu walitelekeza
ushauri wa kuondoka katika maeneo hayo.
Mwanamke mmoja
ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema:: “Nimejua kuhusu ghasia hizo na kifo
cha mwandishi wa habari kijijini kwetu baada ya kurejea nyumbani jioni.”
Kutokana na uvumi wa vitisho uliosambazwa Jumamosi Septemba 1st, 2012, nilipanga
kumtembelea jamaa yangu aliye mbali kama njia ya kuepuka”.
7.5 Mauaji ya
David Mwangosi
Baada ya
kumaliza ukusanyaji wa habari kwa amani katika enelo la utulivu [A], waandishi
wa habari walikwenda katika eneo ambalo liligeuka kuwa mtego wa kifo Eneo la
Umwagaji damu [B] kutoka mwelekeo wa kusini mashariki kupita barabara kuu ya
Dar-Tunduma kumalizia kazia yao.
Alipoangalia
nyuma , Daudi Mwangosi aliona kikundi cha polisi wakimpiga mwandishi mkuu wa
gazeti la Nipashe, wa Iringa, Godfrey Mushi (32).
Mwandisi huyo
alipigwa mpaka akapoteza fahamu na akapata fahamu akiwa kwenye kituo cha polisi
cha Mafinga. Kamera yake, daftari lake na kalamu havikupatiakana.
Wakati mwandishi
Godfrey Mushi akiwa bado anapigwa na polisi, marehemu Mwangosi aliwakimbilia
akiwaomba waache kumdhuru zaidi Mushi kwa kuwa alikuwa mwandishi
tu.
Polisi
hawakumsikiliza. Badala yake wakamburuta mwandishi huyo ambaye tayari alikuwa
amepoteza fahamu na kumweka kwenye gari lao na wakamgeukiwa Daudi Mwangosi
mwenyewe, kwa vurugu na mabmu ya machozi, na kwanza akapoteza
fahamu.
Baada ya kuona
hivyo, Addallah Said mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima akamkimbilia RPC
ambaye alikuwa katika gari lake la polisi aina ya Land Cruiser kumuomba awaamuru
askari waache kumpiga mwandishi Daudi Mwangosi.
Wakati huo huo,
inaelekea kutokana na kushangazwa na polisi kumpiga kinyama Daudi Mwangosi, Mkuu
wa polisi wa Mafinga OCD Asseri Mwampamba, aliamua kuingilia , kwanza kwa
kuwaamuru na kuwaomba askari waache kumpiga marehemu Mwangosi.
Mwandisi wa ITV,
Renatus Mutabuzi ambaye alirekodi tukio hilo “laivu” alithibitisha kwa timu ya
wachunguzi kuwa licha ya jitihada za OCD Asseri kuingilia na kumlinda Mwangosi
kutokana na kipigo, polisi hao hawakumsikiliza.
Wakati polisi
wakiendelea kumpiga Mwangosi, alijaribu kujiokoa kwa kumkumbatia OCD Asseri
Mwampamba, na baadaye kumwangukia miguuni mwake kuepuka kipigo
zaidi.
Baadhi ya
waandishi wa Iringa waliokuwa wamejificha waliweza kupiga picha za mgando na pia
za video za vurugu hizo. Waandishi kutoka Dar es Salaam waliweza kukusanya
habari za vurugu hizo kwa sababu tofauti na wenzao wa Iringa, polisi
hawakuwalenga.
Mwanamke ambaye
alijeruhiwa katika vurugu hizo, aliyekuwepo kwenye eneo hilo la umwangaji damu B
alisema kuwa alilala karibu na ambapo Daudi Mwangosi aliuawa ili kuepuka kipigo
zaidi kutoka kwa FFU.
Alizungumza na
timu ya uchunguzi kwa sharti la kutotajawa. Mwanamke huyo anadai kuwa aliangalia
na hata alimsikia mwandishi Addallah Said akikikimbilia gari la RPC na kumuomba
awaamuru askari wasiendelea kumpiga Daudi Mwangosi.
Alijeruhiwa
vibaya na alilazwa kwenye hospitali ya wilaya ya Mafinga kwa siku tatu. RPC
hakutekeleza ombi la mwandishi huyo. Badala yake alifunga kioo cha gari lake .
Sekunde chache baadaye gari lake lilipiga honi na wakati huo huo mlipuko wa bomu
la machozi ukasikika na kumua mara moja Daudi Mwangosi.
Kwa sababu
marehemu Mwangosi alikuwa bado chini ya miguu ya OCD Asseri Mwampamba, naye pia
alijeruhiwa katika mlipuko huo.
Picha za mgando
zinaonyesha polisi akipiga bomu la machozi tumboni mwa Daudi kwa karibu
kabisa.
Kwa masikito
makubwa, mwanamke huyo anasema alijua kabisa Daudi Mwangosi ameuawa mbele ya RPC
Michael Kamuhanda.
Kwa Addallah
Said na yule mwanamke , kupigwa kwa honi na kutokea kwa mlipuko kwa wakati mmoja
bado ni kitendawili.
Kwa kutoamini
kilichotokea, , OCD Asseri Mwampamba alilalama kwa uchungu kutokana na mlipuko
wa bomu la machozi akisema: “Sasa,umefanya nini ”?
7.6 Taarifa
rasmi zinazokinzana
Taarifa rasmi
lakini zinazokinzana za polisi kuhusu kuuawa kwa David Mwangosi zilipatikana kwa
vyombo mbalimbali vya habari kuanzia Septemba 3, 2012. Mamlaka rasmi hazijafuta
taarifa hizo mpaka wakati wa kuchapisha taarifa hii.
Taarifa hizo,
vyanzo maalum na vyombo mbalimbali vya habari vilivyoandika habari hizo
vinaorodheshwa kama ifuatavyo:
Taarifa rasmi
kwa vyombo vya habari Taarifa (s) Mwangosi afariki kutokana na kitu kizito
kilichotupwa na waandamanaji
• Polisi
wakanusha kuhusika moja kwa moja na kifo cha mwandishi
• Uchunguzi wa
pamoja wa Polisi na Jeshi utafanywa kutokana na kifo cha mwandishi.
• Baada ya
kuvunjwa kwa ghasia, Mwangosi anakimbilia walipo polisi na kitu kama
bomu
kikarushwa kundi
la watu wanaokimbia na kumlipua Mwangosi.
• Watu kadhaa
wengine walijeruhiwa wakiwemo polisi.
• Siko katika
nafasi ya kuzungumza kwa sababu sasa hivi niko katika chumba cha maiti cha
hospitali ya mkoa ya Iringa.
• Akanusha
kuthibitisha kifo lakini athibitisha mtu mmoja amekufa.
• Athibitisha
kifo cha mtu mmoja lakini hana uhakika kama aliyekufa ni mwandishi wa Channel
Ten Chanzo RPC wa Iringa Michael Kamuhanda Kamishna wa Operesheni wa Polisi Paul
Chagonja Taarifa zimepatikana kutoka Polisi makao makuu RPC wa Iringa Michael
Kamuhanda
RPC Michael
Kamuhanda Chombo cha habari / Tarehe/Toleo Na.
• Kamati ya
Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ). 3/09/2012 Mtandao
• Matangazo ya
Channel Ten, asubuhi ya Septemba 3, 2012 Reuters 4/09/2012 mtandao Habari Leo
03/09/2012 02083 1-habari kiongozi Uk. 1
• Matangazo ya
Channel Ten asubuhi ya Septemba 3, 2012 The Daily News 3/09/2012
10726
Habari kuu
Gazeti la Nipashe linanukuu Channel Ten
• RPC anakataa
kuzungumza akisema alikuwa kwenye mkutano • Akanusha madai kuwa
polisi
wamemuua
mwandishi.
•
Kilichosababishakifo ni kitu kilichorushwa na kundi la watu. Polisi
wanachunguza.
• Polisi ilikuwa
ikitawanya kundi la watu. Mwandishi alikuwa akikimbia kutoka kundi la
watu
akifuata polisi.
Kitu hicho pia kilijeruhi watu wengine na baadhi ya maofisa wa polisi akiwemo
OCS.
• Hawatachukua
muda mrefu kukamiklisha uchunguzi kwa sababu mashahidi wengi
wanajulikana.
• Mwili wa
Mwangosi umechukuliwa kwa uchunguzi • Mwandishi aliuawa na bomu la machozi
ambalo halikuwa limeshughulikiwa vizuri na polisi
• Hatutakuwa
katika nafasi ya kusema nani anahusika na mauaji hayo timu mbili za uchunguzi
zitakapokamilisha kazi zake. Hapo ndipo hatua za kisheria zinapoweza
kuchukuliwa.
Msemaji wa
polisi Advera Senso Mkurugenzi Mkuu wa Upelelezi DCI Robert Manumba Waziri wa
Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi (alikariri na Katibu Mtendaji wa Baraza
la
Habar Tanzanika
(MCT) Kajubi Mukajanga)
Dk. Emmanuel
Nchimbi – Waziri wa Mambo ya Ndani Gazeti la Nipashe 03/09/2012
03/09/2012
Habari kuu Gazeti la Mwananchi 03/09/2012 Habari Kuu The Daily News
04/09/2012 Uk.
Wa kwanza habari ndogo Habari Leo 04/09/2012 02084 Habari Kuu
Daily News
05/09/2012 10, 728 Habari ya pili kwa ukubwa (mbele)
7.7 Taarifa
rasmi katika muktadha
Kwa upande mmoja
Waziri wa Mambo ya Ndani anakiri 4/09/2012 kwamba Daudi Mwangosi aliuawa na bomu
la machozi ambalo halikuwa limeshughulikiwa vizuri, siku inayofuata RPC wa
Iringa anatokea kwenye televisheni akitangaza habari za kuwatupia lawama wafuasi
wa Chadema kwa kutupa kitu kizito kilicholipuka na kumuua Mwanjisi, kujeruhi
watu
kadhaa wakiwemo
maofisa wa Polisi.
Mashuhuda na
mambo kadhaa yaliyochukuliwa kwa video na picha mgando zinaonyesha kuwa hakukuwa
na kundi la watu bali ni wanahabari na baadhi ya viongozi wa Chadema ambao
walikuwa wachache kulinganisha na idadi ya polisi. Hata hivyo RPC anadai kuwa
kuiikuwa na
kundi la watu
wakifanya vurugu.
Pia polisi na
taarifa zingine rasmi zimeacha kueleza kuwa tukio la ufunguzi wa tawi
lilifanyika katika eneo tulivu A bila ghasia.
Septemba 12,
2012 Konstebo wa Polisi, Cleophase Pasifious Simon (23) alifikishwa mahakamani
kwa akituhumiwa kwa mauaji ya Mwangosi.
.Ushahidi
unaonyesha kuwa marehemu Mwangosi alikuwa amezingirwa na akipigwa na polisi
wasiopungua saba. Polisi mmoja akiwa amelenga bunduki la kupigia bomu la machozi
tumboni mwa Mwangosi.
Kukamatwa kwa
Konstebo wa polisi na kushitakiwa kunathibitisha Waziri wa Mambo ya Ndani
alichomwambia Katibu Mtendaji wa MCT kuhusu bomu la machozi “kutokushughulikiwa
vizuri” kinyume na jitihada za kuficha ukweli za RPC wa Iringa, Michael
Kamuhanda na maofisa wa polisi wa makao makuu ya polisi mjini Dar es
Salaam.
Cha kushangaza,
wakati akihutubia mkutano wa wanahabari uliovunjika mjini Iringa Septemba 5,
2012 , Mkurugenzi wa Upepelezi wa Makosa ya Jinai, (DCI), Robert Manumba alisema
“matukio ya aina hii yapo na yataendelea kutokea”. Matamshi haya yalitangazwa
sana na vyombo vya habari. Manumba alikuwa akijaribu kuwasihi wanahabari wa
Iringa ambao
waligomea
mkutano aliouitisha mpaka maofisa wote wa polisi wa Iringa waondoke kwenye
ukumbi waliokuwemo. Mgomo huu ulichukuliwa kufuatia uamuzi wa IPC kugomea
kuandika habari za polisi mkoani humo mpaka uchunguzi kuhusu kuuawa ukamilike
Daudi Mwangosi.
8.0 Iliyobaki
yote ni historia
Kilichowashangaza
waandishi katika hatua hii ni kwamba ghafla polisi waliwageuka. Hata baada ya
kuona kuwa mambo yamekuwa mabaya na kukimbia kujifisha kwenye vichaka vya
karibu, polisi waliwafuata na kuwalenga kwa mabomu ya machozi huku
wakikimbia.
Francis Godwin,
mwandishi wa kujitegema, shuhuda na Naibu Katibu Mkuu wa IPC anakumbuka kuwa
polisi wawili walimfukuza mpaka kwenye vichaka vya kijiji cha Nyololo ambapo
alilazimika kuacha gari lake na kurejea usiku kulifuata.
Wakiwa katika
sehemu walipojificha, waandishi walikuwa wakimsaidia Abdallah Said kuondoa
vipande vya nyama ya binadamu vilivyompata kutoka katika mwili wa Daudi
Mwangosi.
Baada ya mkutano
wa waandishi wa habari wa asubuhi katika ofisi za RPC, waandishi waliokuwepo
wanakumbuka kuwa askari mmoja mpelelezi alimfuata Mwangosi na kumwambia : “Ina
maana gani kwenda Nyololo kuandika habari za shughuli za Chadema ambazo zinaweza
kuishia na kifo chako”? Akiwa anatabasamu, Mwangosi alisema: “ nikifa leo ,
mwili wangu
hautazikwa
ardhini lakini katika mioyo ya watu”. Ilikuwa kama vile anatabiri kifo
chake.
Katibu wa IPC
Frank Leonard haelewi kwanini polisi waliwageuka wandishi wenzake.
“Kila siku saa tano asubuhi , tunashiriki
katika mkutano wa waandishi wa habari unaoitishwa na RPC ofisini kwake. Sisi na
maofisa wake tunajua sana na hata kwa majina. Ni kitendawili kikubwa Polisi
wamewashambulia waandishi wakiwa kazini na hatimaye kumuua Daudi
Mwangosi”.
Katika eneo moja
[A], kulikuwa na utulivu ambapo vurugu na umwagaji damu haukuwepo ambapo katika
eneo lingine [B], polisi walitumia nguvu ya ziada, kupelekea kuuawa kwa Daudi
Mwangosi na kujeruhiwa makada wengine kadhaa wa Chadema.
9.0 Shutuma na
kulaaniwa kwa hapa nchini na kimataifa
MCT
Baraza la Habari
Tanzania (MCT) limelaani vikali tukio hilo ambalo ni tishio la moja kwa moja kwa
uhuru wa vyombo vya habari. “Hili ni tukio la kwanza kwa mwandishi wa habari
kuuawa akiwa kazini”, Katibu Mtendaji wa alikaririwa na vyombo vingi vya habari
akisema.
MCT inataka
mamlaka husika kufanya kila liwezekanlo kuhakikisha kuwa ukweli wa kilichotokea
katika siku ya mauaji hayo ya kikatili unajulikana. MCT imeshutumu kuwahusisha
wanahabari na shughuli za kisiasa na kumuhusisha na chama cha siasa wakati
alikuwa akifanya kazi yake UTPC
Taarifa ya Umoja
wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)umeshutumu vikali mauaji ya Daudi
Mwangosi mikononi mwa polisi wakati akitekeleza kazi zake kama mwandishi wa
habari. Taarifa hiyo imeitaka serikali kuwawajibisha mara moja polisi
waliohusika na operesheni iliyopelekea kifo cha Mwangosi.
UTPC imetaka
kufukuzwa kazi mara moja kwa maofisa waliohusika na kifo marehemu Daudi
Mwangosi.
Jukwaa la
Wahariri Tanzania (TEF) Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limelaani vikali
mauaji ya Mwangosi mikononi mwa polisi.
Katibu Mkuu wa
TEF, Neville Meena, anasema hii ni mara ya kwanza katika historia ya sasa
Tanzania kwa mwandishi kuuawa akiwa kazini.
MISA na
wengine
Taasisi ya
Vyombo vya Habari ya Kusini mwa Afrika (MISA), Kamati ya Kulinda Waandishi wa
Habari (CPJ) na ARTICLE 19, zote zimelaani kuuawa kwa Daudi Mwangosi akiwa
mikononi mwa polisi.
Levi Kabwato,
ofisa Programu wa MISA anayeshughulikia Ufuatiliaji wa Uhuru wa Vyombo vya
Habari na Utafiti, alieleza katika taarifa kustushwa kwake na mauaji ya
Mwangosi.
“Hii inastusha.
Septemba 2 2012, si siku mbaya kwa uandishi wa habari wa Tanzania bali kwa eneo
zima na dunia yote. Ghasia siyo jibu, hazitatui kitu.
Tunaitaka
serikali ya Tanzania kuanzisha uchunguzi na kuwawajibisha wote waliohusika na
upotefu wa maisha,” Kabwato alisema katika taarifa.
CPJ inasema
kwamba kifo cha Mwangosi ni cha kwanza kwa mwanahabari aliye kazini nchini
Tanzania tangu taasisi hiyo ilipoanza kuweka rekodi za kina 1992
ARTICLE 19
imeeleza kusikitishwa na mauaji ya Daudi Mwangosi mikononi mwa Polisi wa
Tanzania, na kuitaka serikali ihakikishe wote waliohusika
wanashitakiwa.
Unesco
Mkurugenzi Mkuu
wa UNESCO, Irina Bokova, pia alishutumu mauaji ya mwandishi wa habari wa
Tanzania, Daudi Mwangosi Septemba2, 2012 na kuitaka serikali kuchunguza mauaji
hayo.
UNESCO inataka
serikali ichunguze kifo hicho na kuwashitaki wote wanaohusika.
Taarifa ya
UNESCO inasema: “ Ni muhimu kwa demokrasi na utawala wa sheria kwamba waandishi
waruhusiwe kufanyakazi zao na kutumia haki yao ya kujieleza kwa
usalama.”
10.0 Hitimisho
na Mapendekezo Mauaji ya David Mwangosi mikononi mwa polisi wakati akiwa kazini
ni tishio kwa uhuru wa habari.
Uhuru wa habari
ni kumwezesha waandishi kufanyakazi bila vitisho ama ghasia na waweze kuripoti
wakiwa huru bila kudhibitiwa.
Kama mwandishi,
Daudi Mwangosi alikuwa akitimiza haki yake ya kikatiba kufanya “kazi nzuri”.
Kwa vyombo vya
habari na hasa waandishi, haijalishi kama Kamanda wa Mkoa wa Polisi ameipiga
marufuku shughuli za Chadema katika kijiji cha Nyalolo au la.
Ilikuwa ni jambo
ka maslahi ya umma kwa vyombo vya habari ambalo vyombo vya habari vilistahili
kuripoti kadri mambo yalivyokuwa yaakiendelea na watu wenyewe kufanya
uamuzi.
Kimsingi, wakati
wote na katika matukio yote, mazuri ama mabaya, waandishi lazima wawepo na
wachukuliwe kama watu wasio na upande wowte.
Pia, Polisi
walitumia nguvu ya ziada bila sababu dhidi ya watu wasio na silaha katika kijiji
cha Nyololo village.Katika hatua ya mwisho, ikawa vita ya polisi dhidi ya
waandishi wa habari na hatimaye kuuawa kwa Daudi Mwangosi.
Timu ya
uchunguzi haikubali kabisa suala la kukosea utambulisho wa mtu. Waandishi wanane
waliokuwep katika kijiji cha Nyololo waliweza kutambulika kwa urahisi, hasa
kutokana na mambo kwenda salama katika eneo la uslamaa [A].
Waandishi
walikuwa na Kamera, vidaftari na kalamu na wengine kama sio wote walikuwa
wanafahamika sana na polisi wa Iringa.
Sasa imebainika
wazi kwamba Polisi walikuwa wanawawinda waandishi wa Iringa ambao walikuwa
wakiwajua.
Mapambano ya
Chadema na Polisi katika Kijiji cha Nyololo habari zake zilikusanywa na
waandishi kutoka Dar es Salaam pia. Kwanini walikuwa waandishi wa Iringa ndiyo
walilengwa katika ghasia hizo.!
Uhasama na chuki
iliyokuwepo kati ya RPC wa Iringa na marehemu Daudi Mwangosi katika kipindi
chote cha saa kadhaa tangu mkutano wa waandishi wa habaria na dakika chache
kabla ya mauaji yake mbele ya RPC huyo huyo katika kijiji cha Nyololo Septemba
2, 2012 unaibua maswali mengi kuliko majibu.
Waandishi sita
wa Iringa wameathirika na msongo wa mawazo kutokana na kiwango cha ghasia
walizofanyiwa na polisi na wanafikiria kuachana na kazi ya uandishi. Mmoja
anapanga kuwa mchungaji kwa kuhofia maisha yake.
Mamlaka husika
zahitaji kuwa na mipango ya kuwaelimisha polisi jinsi ya kushughulika na vyombo
vya habari hasa na wandishi wa habari. Lengo liwe kuboresha mahusiano ya kikao
kati ya pande hizo mbili..
Hii inatokana na
uhusiano mbaya iliyoibuka kati ya waandishi wa Iringa na polisi wa mkoa tgangu
robo ya mwisho wa 2011. Uhusiano huu kati ya pande hizi mbili umekua tangu 2011
ambapo aliyekuwa OCD wa Iringa Mohamed Semunyu alipoamriwa ana bosi wake kulipa
kamera ya mwandishi aliyoiharibu bila sababu ya maana.
Inashinda
ufahamu wa kawaida kwamba matukio mawili ya yanayofanana katika siku moja
ynashughulikiwa tofauti.: Moja linashughulikiwa na ukatili na nguvu kubwa kwa
kuwalenga wanahabari wa Iringa.
Katika tukio la
kwanza, RCO aliamua Chadema wanaweza kuendelea na masuala yao ya ndani katika
ofisi yao na katika tukio la pili Mkuu wa polisi wa mkoa anaamua shughuli hizo
zisimamishwe kwa vyovyote na hata kwa nguvu.
Akigusia kwa
kiasi mpambano wa Nyololo kati ya Polisi na wafuasi wa Chadema, Rais Jakaya
Kikwete katika hotba yake ya kila mwezi kwa taifa kwa mwezi wa September 2012,
alisisitiza polisi kuepuka matumizi ya nguvu za kupita kiasi na kuwakumbusha
watanzania na wanasiasa
kuheshimu sheria
za nchi na kuiona polisi kama wasimamizi wa amani na usalama.
Rais alifafanua
kuwa Jeshi la Polisi lina mamlaka ya kuruhusu au kuzuia haki ya kufanya mikutano
na maandamano ya vyama vya siasa.
Taarifa za awali
za maofisa wa ngazi za juu kuhusu mauaji ya M wangosi zilitofautiana na mtu
anapoziangalia kutokana na ushahidi uliopatikana ni dhahiri kulikuwa na jitihada
za kuficha ukweli.
Tukio hilo
limeharibu sifa ya Tanzania kimataifa kama nchi ya amani na ya
demokrasia.
Mauaji ya
Mwangosi yalitokea wakati wa kufanyika mkutano wa Chama cha Umoja wa Mabaraza ya
Habari Duniani (WAPC) ambapo MCT ilikuwa mwenyeji wake.
Katibu Mkuu wa
WAPC, Chris Conybeare, alimwambia waziri wa Habari, Dk. Fenella Mukangara:
“Wakati waandisi wanauawa demokrasi pia inakufa.. tukio hili moja limeanza
kuichafua sifa yaTanzania ya kuendeleza uhuru wa habari”.
Zaidi ya Polisi
saba chini ya uongozi wa RPC Michael Kamuhanda kwa pamoja wamemzingira na
kumpiga Daudi Mwangosi. Kwanini wengine hawajashitakiwa, si suala linalohitaji
uelewa wa kawaida.
Hata hivyo
uchunguzi hauwezi kuthibitisha kama mauaji hayo ya Mwangosi
yalipangwa.
11.0 Picha za
mauaji ya Daudi Mwangosi
Daudi Mwangosi
akiwa mwenye furaha (kaka mduara) waka akimhoji Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Iringa, Michael Kamuhanda (kulia) kaka kijiji cha Nyololo muda mfupi kabla ya
mauaji yake.
Askari wa kikosi
cha FFU wakiwa wamejiandaa katika kijiji cha Nyololo Polisi wakiwa
Wamemzingira na
wakimpiga vibaya mwandishi Daudi Mwangosi. Aliuawa hapo
hapo.
No comments:
Post a Comment