TANGAZO


Monday, October 22, 2012

Wafanyakazi wapya Benki ya Posta wapigwa msasa, Mkurugenzi Mtendaji Moshingi afungua mafunzo yao


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kushoto), akijadili jambo na Mkurugenzi wa Majanga wa benki hiyo, Moses Manyatta, mara baada ya kuifungua semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo waajiriwa wapya wa benki hiyo, iliyoanza leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Baadhi ya waajiri wa wapya wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Rasilimali watu, Peter Mapigano (hayupo pichani), wakati alipokuwa akiwasilisha mada kwa wafanyakazi hao katika semina yao ya siku nne ya mafunzo ya kuwajengea uwezo, iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
 
Baadhi ya waajiriwa wapya wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Rasilimali watu, Peter Mapigano (hayupo pichani), wakati alipokuwa akiwasilisha mada kwa wafanyakazi hao, katika semina yao ya siku nne ya mafunzo ya kuwajengea uwezo, Dar es Salaam leo.

 
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Peter Mapigano, akiwasilisha mada kuhusu uwajibikaji katika kazi kwa wafanyakazi hao, katika semina yao ya siku nne ya mafunzo ya kuwajengea uwezo, iliyofanyika katika ukumbi wa Luther House, Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Peter Mapigano,  akifafanua masuala mbalimbali kwa wafanyakazi hao wapya katika semina yao ya siku nne ya mafunzo ya kuwajengea uwezo, iliyofanyika katika ukumbi wa jengo la Luther House, Dar es Salaam leo.


Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Andrew Chimazi, akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya masoko katika benki, wakati wa semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo waajiriwa wapya wa benki hiyo, Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (katikati mbele waliokaa), akipiga picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi na waajiriwa wapya wa benki hiyo, mara baada ya kuifungua semina yao ya siku nne ya mafunzo ya kuwajengea uwezo waajiriwa hao wapya, Dar es Salaam leo.

Baadhi ya waajiriwa wapya wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mikopo wa benki hiyo, Michael Mwakyandile (hayupo pichani), wakati alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu watu gani wanaostahiki kupewa mikopo, katika semina yao ya siku nne ya mafunzo ya kuwajengea uwezo, Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Michael Mwakyandile (pichani), akiwasilisha mada kuhusu watu gani wanaostahiki kupewa mikopo, katika semina ya siku nne ya mafunzo ya kuwajengea uwezo, waajiriwa wapya wa benki hiyo, Dar es Salaam leo.

Baadhi ya waajiriwa wapya wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), wakimsikiliza Mkurugenzi wa  Fedha wa benki hiyo, Mauro Mhule (hayupo pichani), wakati alipokuwa akiwasilisha mada inayohusu masuala ya fedha katika semina yao siku nne ya mafunzo ya kuwajengea uwezo, Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Mauro Mhule, akiwasilisha mada inayohusu masuala ya fedha katika semina ya siku nne ya mafunzo ya kuwajengea uwezo, waajiriwa wapya wa benki hiyo, iliyoanza leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment