TANGAZO


Friday, October 12, 2012

Vurugu za Mbagala kati ya Polisi na Waislamu


Kisa mtoto kuikojolea Quraan na kumdunda mtoto wa madrassa.
Asakari wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha FFU wakiruka mtaro na watuhumiwa wavurugu zilizo zuka leo kwenye eneo la Mbagala Kizuiani baada ya mtoto anaedaiwa kuwa wa kidato cha kwanza kudaiwa kuikojolea Qurani Tukufu na kusababisha taharuki kubwa mchana wote wa leo, ambapo hadi jioni Mbagala ilikuwa bado vurugu zikiendelea.

Baadhi ya watu waliokuwa katika shughuli zao kwenye eneo hilo, walishindwa kuendelea na shughuli hizo, kufuatia vurugu hizo. Mama huyu pichani alikua anatoka Msikitini kuswali swala ya Ijumaa, lakini akakutana na dhahama ya mabomu na kulazimika kukimbia.
Baadhi ya vijana wanaodaiwa kuendesha vurugu hizo, wakipandishwa kwenye gari la polisi eneo la Kizuiani baada ya kutiwa mbarouni na maafande hao.
Hapa Askari wakiwakimbilia vijana waliokuwa wamevalia kanzu na kofia huku wakiwatafuta wabaya wao kwa alama za kanzu na sijida kwenye paji la uso, ambapo ilikuwa ni vigumu kwa watu ama vijana waliokuwa na alama hizo kusalimika kutiwa nguvuni.
Waislamu hapa walisimbana na Polisi hao na kazi ikawa piga nikupige kati ya askari hao na waislamu ana kwa ana, ambapo mabomu, virungu kamwe vingeweza kufanyakazi kwani vijana hao walikuja kwa nguvu kubwa, wakitaka kuvamia kituo cha Polisi cha Maturubai, katika eneo hilo la Kizuiani.
Hapa ikawa piga nikupige tu hadi askari hao kufanikiwa baadhi ya vijana hao kuwatia nguvuni huku wakiwapa kisago cha nguvu.
Hawa ni baadhi ya vijana waliokamatwa kwenye vichochoro mbalimbali vya eneo hilo baada ya kukimbia mabomu na kujificha.

Hii ndio hali halisi ilivyokuwa kamata piga, kamata piga, peleka kwenye gari na kisha kupelekwa kwenye vituo vya Polisi kuhifadhiwa. Wananchi hawa waliamua kukaa chini ili kusalimu amri lakini hiyo haikuwaponya kwani virungu vilitua vichwani mwao mpaka basi. 
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo, wakizungumza na waandishi wa habari, kulalamikia mabomu na kudai kuwa yalikuwa yakiwaumiza sana kwani mchana kutwa wa leo, hali ilikuwa ni mbaya hasa ikizingatiwa watoto walikuwa wamelazwa majumbani na hivyo kuathiriwa na mabomu hayo.
Hili ni moja kati ya Makanisa matatu yaliyovunjwa vioo, hapa baadhi ya waandishi wa habari wakiangalia vioo vilivyovunjwa kwenye kanisa hilo jipya la Wasabato lililopo upande wa magharibi karibu na kituo cha mabasi cha Kizuiani Mbagala.
Barabara zilifungwa kwa mawe na mapipa huku askari kupata wakati mgumu kupita katika maeneo hayo.
Hapa moto ukiwaka katikati ya barabara, ambapo matariri yatumika kuuwasha moto huo.

Vijana wa umri huu ndio walikuwa wakiwahenyesha Polisi kwa muda wote kwani ni wajanja na wanakimbia sana.

Moto ukiwaka na magari kushindwa kupita katika maeneo hayo.

Polisi wakiwaingiza kwenye gari, vijana waliowanasa kwenye vurugu hizo.

Mtuhumiowa akipandishwa kutoka kwenye mtaro kuelekea kwenye gari. (Kwa hisani ya Raha za Pwani)

No comments:

Post a Comment