Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu akitoa maoni yake kwenye mkutano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (hayupo pichani), jijini Tokyo- Japan.
Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa (wa pili kulia), akiwa na ujumbe wake katika mkutano huo. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona, akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Siyvacius Likwelile na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar, Khamisi Mussa Omari katika mkutano huo, jijini Tokyo- Japan.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Bara la Afrika, Bw. Makhtar Diop (wa pili kulia), akiwa ameambatana na Maofisa Waandamizi kutoka Benki ya Dunia wakati wa mazungumzo na Waziri wa Fedha, William Mgimwa (hayupo pichani) katika mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Bara la Afrika, Makhtar Diop (katikati), akifurahia jambo, wakati wa mazungumzo na Waziri wa Fedha, William Mgimwa (hayupo picha) katika mkutano huo.
Waziri wa fedha, William Mgimwa, akifafanua jambo kwa Ofisa wa Benki ya Dunia.
Ujumbe kutoka Tanzania, ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa pamoja na Maofisa kutoka Benki ya Dunia wakiendelea na majadiliano juu ya kuangalia uwezekano wa kuisaidia Tanzania ili iweze kendelea kiuchumi hapa jijini Tokyo- Japan.
Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa (wa pili kushoto), akiwa na ujumbe wake katika mkutano huo. |
Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa pamoja na Maofisa kutoka Benki ya Dunia, wakiendelea na majadiliano juu ya kuangalia uwezekano wa kuisaidia Tanzania ili iweze kendelea kiuchumi, hapa Jijini Tokyo- Japan.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Bara la Afrika, Makhtar Diop, akiwa ameambatana na Maofisa Waandamizi kutoka Benki ya Dunia, wakati wa mazungumzo na Waziri wa Fedha, William Mgimwa ambaye yuko na ujumbe wake kutika Tanzania pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona katika kikao cha pamoja ambacho Waziri Mgimwa alikutana na Kiongozi huyo kwa madhumuni ya kutoa mapendekezo ya maeneo ambayo Tanzania ikisaidiwa itasonga mbele kiuchumi.
Kushoto kwa Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu ni Maafisa kwa Benki ya Dunia wakifuatilia kwa makini kuhusu mkutano huo wakiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania hapa Jijini Tokyo – Japan. (Picha zote na Ingiahedi Mduma-Wizara ya Fedha)
No comments:
Post a Comment