Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, wakijiandikisha kupata huduma za Afya, katika kambi maalum ya utoaji wa huduma za afya iliyoandaliwa na Chama cha Wanafunzi Madaktari na kufadhiliwa na Vodacom, mwishoni mwa wiki hii. Huduma hiyo ya matibabu inatolewa bure katika kijiji cha Magawa, wilayani Mkuranga.
Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation, akizungumza na akina mama wa Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, waliojitokeza kupata matibabu katika kambi maalum iliyoadhiliwa na Chama cha Madaktari wanafunzi Tanzania na kufadhiliwa na Vodacom Foundation mwisho wa wiki. Huduma hizo za afya zinatolewa bure katika kijiji cha Magawa.
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, wakipata huduma za matibabu katika kambi maalum iliyoandaliwa na Chama cha Madaktari Wanafunzi Tanzania na kufadhiliwa na Vodacom Foundation. Matibabu hayo yatatolewa bure katika kijiji cha Magawa wilayani humo. (Na mpigapicha wetu)
No comments:
Post a Comment