Katibu wa Jumuiya ya Shura ya Maimamu Tanzania , Sheikh Ponda Issa Ponda (mwenye
kanzu), akiwa chini ya ulinzi mkali wa Askari Polisi, wakati akitoka katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo, baada ya kusomewa mashtaka ya
wizi, uvunjifu wa amani na uchochezi.
Katibu wa Jumuiya ya Shura ya Maimamu Tanzania , Sheikh Ponda Issa Ponda, akishuka katika gari lililomleta katika Mahakama ya
Kisutu, Dar es Salaam leo.
Katibu wa Jumuiya ya Shura ya Maimamu Tanzania , Sheikh Ponda Issa Ponda (mwenye kanzu nyeupe mbele), akiwa katiika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, alikofikishwa pamoja na wafuasi wanaomuunga mkono, kama
wanavyoonekana pichani kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili ya Uchochezi, wizi na Uvunjifu wa Aman, Dar es Salaam jana. (Picha zote na Habari Mseto)
Katibu wa Jumuiya ya Shura ya Maimamu Tanzania , Sheikh Ponda Issa Ponda (mwenye kanzu nyeupe mbele), akiwa katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili, Dar es Salaam leo.
Hali ya ulinzi ilikuwa kama inavyoonekana,
ambapo askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU), walikuwa wakilinda amani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Askari wa Kikosi cha Kuzuiya Ghasia, wakiwa kwenye gari lao, wakiwa tayari kwa lolote kwa ajili ya kulinda usalama kwenye Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam leo, wakati Katibu wa Jumuiya ya Shura ya Maimamu
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakitawanyika baada ya Sheikh Ponda na wafuasi
wake kurejeshwa mahabusu.
Sheikh Ponda akipanda gari kurejeshwa mahabusu. |
KATIBU wa Jumuiya ya Shura ya Maimamu Tanzania , Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasi wake 49 leo, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu jijiji hapa
kwa kosa la uchochezi na wizi wa mali zenye thamani ya
Shilingi milioni 59.
Wakati wakifikishwa na baadaye kuondoka kwenye
viwanja vya mahakama hiyo wakiwa ndani ya magari ya Polisi na Jeshi la Magereza,
walikuwa wakisikika wakipaza sauti wakisema; ‘Allah Akbar, Allah
Akbar’.
Sheikh Ponda pia amefikishwa mahakamani hapo akidaiwa
kuwashawishi Waislamu kugomea zoezi la sensa ya watu na makazi, iliyofanyika
mwezi uliopita nchini kote na kufanya zoezi hilo kufanyika kwa kusuasua.
Hali ya usalama kwenye mahakama ya Kisutu na maeneo ya
jirani iliimarishwa mchana wa leo, wakati Sheikh Ponda aliyekamatwa jana na
Jeshi la Polisi na kufikishwa Makao Makuu ya Jeshi hilo katikati ya jiji –
akifikishwa hapo na Waislamu wengine walioshiriki uvamizi wa kiwanja
Chang’ombe.
Baada ya kukamatwa juzi usiku na kufikishwa Kituo Kiuu cha
Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam jana, baadhi ya Waislamu wanaomuunga mkono
walivamia kituoni hapo kushinikiza kuachiwa kwa kiongozi wao, kabla ya polisi
kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.
Hali ya amani imekuwa tata nchini katika siku za karibu,
tangu Ijumaa iliyopita, ambapo kundi la watu wanaosadikika kuwa ni Waislamu
walivamia kituo cha polisi huko Mbagala Zakhiem wakishinikiza wakabidhiwe kijana
aliyedaiwa kukojolea Msahafu.
Baada ya kushindwa kufanikisha azma hiyo, hasira zao
zikaishia katika uvamizi wa makanisa, ambayo kadhaa yalichomwa moto, kuharibiwa
na kuibiwa kwa vitu mbalimbali na polisi kuwakamata watu zaidi ya 120 kabla ya
kuchujwa na kubaki 36 waliofikishwa mahakamani.
Hali haikuwa shwari pia Visiwani Zanzibar, ambako kikundi
maarufu cha Uamsho kimefanya vurugu jana, wakimskaka kiongozi wao mkuu Sheikh
Farid, aliyedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana juzi usiku.
Kesi ya Sheikh Ponda ambaye alinyimwa dhamana na wenzake
itatajwa tena Novemba Mosi mwaka huu, ambapo watarudi mahakamani hapo.
No comments:
Post a Comment