Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Utawala, Profesa Yunus Mgaya, akizungumza katika hafla ya ufungaji wa wiki ya mafunzo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo hicho, chuoni hapo, leo mchana, ambapo Benki ya Posta Tanzania (TPB), imeyadhamini mafunzo hayo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Baadhi ya viongozi wa UDSM, wakimsikiliza Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, upande wa Utawala, Profesa Yunus Mgaya (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza katika hafla ya ufungaji wa wiki ya mafunzo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza, chuoni hapo leo mchana, ambapo Benki ya Posta Tanzania (TPB), imeyadhamini mafunzo hayo.
Baadhi ya wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza wa UDSM, wakimsikiliza Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, upande wa Utawala, Profesa Yunus Mgaya (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza nao katika hafla ya ufungaji wa wiki yao ya mafunzo, chuoni hapo leo mchana, ambapo Benki ya Posta Tanzania (TPB), imeyadhamini mafunzo hayo.
Baadhi ya wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza wa UDSM, wakifuatilia hotuba ya Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, upande wa Utawala, Profesa Yunus Mgaya (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza nao katika hafla ya ufungaji wa wiki yao ya mafunzo, chuoni hapo leo mchana, ambapo Benki ya Posta Tanzania (TPB), imeyadhamini mafunzo hayo.
Mlezi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Rebecca Sima, akizungumza katika hafla hiyo, iliyodhaminiwa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), chuoni hapo leo.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Allen Mushi, akizungumza katika hafla hiyo ya ufungaji wa wiki ya mafunzo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo.
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Utawala, Profesa Yunus Mgaya (kulia), akiteta jambo na Makamu Mkuu wa chuo hicho, upande wa Taaluma, Profesa Makenya Maboko, wakati wa ufungaji wa wiki hiyo ya mafunzo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza jijini leo.
Baadhi ya wahadhiri, wageni waalikwa na wafanyakazi wa UDSM, wakiwa katika hafla hiyo, iliyodhaminiwa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), chuoni hapo leo.
Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Utawala, Profesa Yunus Mgaya (kulia) na Makamu Mkuu wa chuo, upande wa Taaluma, Profesa Makenya Maboko (katikati), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma wa UDSM, Profesa Allen Mushi, alipokuwa akitetea nao jambo, wakati wa ufungaji wa wiki hiyo ya mafunzo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza jijini leo.
Mlezi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Rebecca Sima, akimtambulisha mmoja wa wafanyakazi wa chuo hicho, Paulina Mabuga, Meneja wa USAB kwa wanafunzi hao.
Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), upande wa Masoko, akigawa vipeperushi vya benki hiyo kwa wanafunzi hao kwa ajili ya kuwapatia maelezo ya huduma na faida mbalimbali zipatikanazo katika benki hiyo, ambapo pia zawadi mbalimbali zilitolewa na benki hiyo kwa wateja waliojiunga nayo leo, wakati wa ufungaji wa wiki hiyo ya mafunzo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza, yaliyodhaminiwa na benki hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), upande wa Masoko, wakijadili jambo kabla ya kugawa vipeperushi na kutoa elimu ya huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo kwa wanafunzi hao leo, wakati wa ufungaji wa wiki hiyo ya mafunzo, chuoni hapo, ambapo benki hiyo iliyadhamini.
Ofisa Mauzo Mwandamizi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Diana Mroso (kushoto), akiwasikiliza baadhi ya wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza, walipotaka kufahamu huduma na faida mbalimbali zinazopatikana kwa kuwa mteja wa benki hiyo, wakati alipokuwa akiwaelimisha kwenye hafla hiyo, ambayo wanafunzi wengi walijiunga na benki hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), upande wa Masoko, wakitoa elimu na kugawa vipeperushi kwa wanafunzi hao.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), upande wa Masoko, wakienda kutoa huduma kwa wanafunzi hao leo, ambao walimiminika kwa wingi kujiunga na benki hiyo katika hafla ya ufungaji wa wiki hiyo ya mafunzo, chuoni hapo, iliyodhaminiwa na benki hiyo.
Baadhi ya wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza wa UDSM, wakijaza fomu za kujiunga na Benki ya Posta Tanzania (TPB) katika hafla ya ufungaji wa wiki yao ya mafunzo, chuoni hapo leo mchana, mafunzo yaliyodhaminiwa na benki hiyo.
Ofisa Masoko wa Benki ya Posta (TPB), Christina Mselewa (kulia), akiwafahamisha baadhi ya wanafunzi hao jinsi ya kujaza fomu za kujiunga na benki hiyo, wakati wa hafla hiyo, chuoni hapo leo.
Baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wakijaza fomu za kujiunga na Benki ya Posta Tanzania (TPB), mara baada ya kufungwa kwa wiki yao ya mafunzo chuoni hapo leo mchana.
Baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wakiwa kwenye ukumbi maalum uliotengwa, wakati wa hafla hiyo, wakijaza fomu za kujiunga na Benki ya Posta Tanzania (TPB), mara baada ya kufungwa kwa wiki yao ya mafunzo chuoni hapo leo mchana.
Baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wakijaza fomu za kujiunga na Benki ya Posta Tanzania (TPB), chuoni hapo leo mchana.
Maofisa wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), wakiangalia picha walizowapiga wateja wao wapya, wakati wakijiunga na benki hiyo kwenye hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko, Andrew Chimazi (katikati), akiwafahamisha jambo baadhi ya Maofisa Masoko wa benki hiyo, wakati wa hafla hiyo kwa ajili ya kuwahudumia wateja wao wapya waliojiunga na benki.
Baadhi ya Maofisa wa Masoko, wakijipumzisha baada ya kazi nzito ya kuwahudumia wateja wao wapya, wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa UDSM waliojiunga na TPB wakati wa hafla hiyo.
Mmoja wa Maofisa wa TPB, akiwapungia wateja wao wapya baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwaingiza kwenye huduma za kibenki zinazopatikana kwenye Benki hiyo, wakati wa hafla ya ufungaji wa wiki ya mafunzo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo leo.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), waliokuwepo katika hafla hiyo, wakijadili jambo baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, wakati wa hafla ya ufungaji wa wiki ya mafunzo kwa wanafunzi hao.
Baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa UDSM, wakichukua zawadi zao, za papo hapo mara baada ya kujiunga na benki hiyo jijini Dar es Salaam leo, wakati wa ufungwaji wa wiki yao ya mafunzo chuoni hapo.
Baadhi ya Maofisa wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), wakijadili jambo, wakati wa hafla hiyo, ambayo benki hiyo, ilidhamini wiki ya mafunzo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), yalifungwa rasmi leo.
Wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), upande wa Masoko, wakipiga picha ya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali vihusikavyo na huduma mbalimbali kwa wateja baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwaingiza wateja wapya katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment