TANGAZO


Monday, October 29, 2012

Twiga Cement yakabidhi zawadi kwa washindi wa Tuzo za Mazingira



 Mkurugenzi wa Idara ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ignace Mchallo (kushoto), akimpongeza  Leonard Gastory Lugali, aliyeibuka mshindi wa kwanza wa shindano la mazingira lililopewa jina la Quarry Life Award, lililokuwa likiendeshwa na Kampuni ya Saruji ya Tanzania Portland Cement (Twiga) na kupewa zawadi ya EURO 5000 katika hafla iliyofanyika kiwandani hapo, Dar es Salaam leo. Mshindi wa pili alipewa EURO 5000 na wa tatu aliondoka na 1500. Wengine pichani ni washindi, majaji wa shindano na maofisa wa TPCC.

 Mkurugenzi wa Idara ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ignace Mchallo (kushoto), akikabidhi mfano wa hundi ya Euro 3000 kwa David Dawson Maleko, akiyeibuka mshindi wa pili wa shindano la mazingira lililopewa jina la Quarry Life Award, lililokuwa likiendeshwa na Kampuni ya Saruji ya Tanzania Portland Cement (Twiga) katika hafla iliyofanyika kiwandani hapo, Dar es Salaam leo.  Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa TPCC, Ignatius Asare, Ofisa Mazingira, David Mwakalobo, Meneja Mazingira wa Twiga, Juliet Mboneko Tibaijuka  na Meneja Mazingira kutoka Heidelberg Cement, Dk Michael Rademacher.

Mkurugenzi wa Idara ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ignace Mchallo (kushoto), akikabidhi cheti kwa Meneja Mazingira wa TPCC, Juliet Mboneko Tibaijuka, mmoa wa watu waliofanikisha mchakato wa tuzo hizo.

 Washindi wa shindano la mazingira lililopewa jina la Quarry Life Award, lililokuwa likiendeshwa na Kampuni ya Saruji ya Tanzania Portland Cement (Twiga), wakiwa wameshikilia vyeti, zawadi na tuzo zao walizokabidhiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ignace Mchallo (hayupo pichani), katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya watu waliohudhuria sherehe za kukabidhi tuzo kwa washindi wa shindano la mazingira lililoandaliwa na Twiga Cement jijini Dar es Salaam leo, wakiwa katika hafla hiyo, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka katika hafla hiyo. (Picha zote na Peter Mgongo) 

No comments:

Post a Comment