Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Abdalla Mwinyi Khamis (kulia), akikabidhi fedha kwa ajili ya ubani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, nyumbani kwa wafiwa wa marehemu Koplo Said Abdulrahman Juma wa Jeshi la Polisi, Nyerere mjini Zanzibar leo kwa niaba ya wanafamilia wa marehemu. Baba Mdogo Juma Omar Salum (wa pili kushoto), akipokea ubani huo. Wa pili kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Said Mwema na kushoto ni Baba mzazi wa marehemu, Abdulrahman Juma Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Abdalla Mwinyi Khamis (kulia), akiagana na baba wa marehemu Koplo Said Abdulrahman Juma wa Jeshi la Polisi, mara baada ya kukabidhi ubani kwa wafiwa kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, nyumbani kwa wafiwa, Nyerere mjini Zanzibar leo.

No comments:
Post a Comment