TANGAZO


Sunday, October 7, 2012

Simba yaisambaratisha JKT Oljoro, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, yaipiga 4-1

 Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu hiyo na JKT Oljoro ya Arusha, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo jioni. Simba ilishinda mabao 4-1. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Paul Ngalema wa Simba (kushoto), akipambana na Yussuf Nachogote wa JKT Oljoro katika mchezo huo. 

Emmanuel Okwi wa Simba (kulia), akikimbia na mpira huku akifuatwa na Yussuf Nachogote wa JKT Oljoro ya Arusha jijini Dar es Salaam leo jioni Uwanja wa Taifa jijini. 

  Emmanuel Okwi wa Simba (kulia), akiwania mpira na Yussuf Nachogote wa JKT Oljoro katika mchezo huo.

 Emmanuel Okwi wa Simba (mbele), akimtoka Yussuf Nachogote wa JKT Oljoro katika mchezo huo.

  Emmanuel Okwi wa Simba (kulia), akiwania mpira na Salim Mbonde wa JKT Oljoro, Uwanja wa Taifa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom jijini Dar es Salaam leo jioni. Simba ilishinda mabao 4-1.

  Yussuf Nachogote wa JKT Oljoro (kulia), akimzidi nguvu Emmanuel Okwi wa Simba wakati wa mchezo huo.

  Emmanuel Okwi wa Simba (kulia), akijaribu kumtoka Yussuf Nachogote wa JKT Oljoro wakati wa mchezo huo.

Wachezaji Emmanuel Okwi wa Simba (kulia) na Yussuf Nachogote wa JKT Oljoro wakipambana kuwania mpira wakati wa mchezo huo.

Mashabiki wa Simba wakishangilia timu yao katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.

Amri Kiemba wa Simba akikimbia na mpira huku akifuatwa na Saleh Idd wa JKT Oljoro.

Amri Kiemba wa Simba akipiga mpira mbele ya Saleh Idd wa JKT Oljoro.

 Somari Kapombe wa Simba, akikokota mpira huku akifuatwa na Jackson Semfukwe.

 Golikipa wa timu ya JKT Oljoro, akimchezea rafu Emmanuel Okwi wa Simba katika mchezo huo na refa kuamua kumtoa nje na kupigwa penalti iliyozaa goli na nne kwa upande wa Simba, lililotiwa kimiani na Felix Sunzu. 

 Felix Sunzu (kushoto) na Kiggi Makasy, kila mmoja akitaka kupiga penalti hiyo, ambayo hatimaye ilipigwa na Sunzu na kuwa goli la nne kwa Simba.

Golikipa aliyechukua nafasi ya Shaibu Issa, akijaribu kuudaka wa penalti, uliopigwa na Sunzu, akijirusha kuudaka bila mafanikio.

No comments:

Post a Comment