Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered, wakishusha magodoro katika kitoa cha kulelea yatima cha Yatima Group Trust Fund, kilichopo Chamazi. Benki hiyo ilitoa msaada wa vitu mbalimbali kwenye kituo hicho kwa ajili ya yatima hao.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered, wakiwa katika picha ya pamoja na yatima wanaolelewa katika kituo cha Yatima Group Trust Fund, kilichopo Chamazi, jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi wa benki hiyo, walienda kutembelea kituoni hapo na kutoa msaada wa vitu mbalimbali.
Wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered, wakiwagawia juisi na biskuti watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea yatima cha Yatima Group Trust Fund, kilichopo Chamazi, mkoani Dar es Salaam leo. Wafanyakazi wa benki hiyo, walienda kutembelea kituoni hapo na kutoa msaada wa vitu mbalimbali.
No comments:
Post a Comment