TANGAZO


Sunday, October 7, 2012

Rick Ross apagawisha Tamasha la Fiesta 2012, Leaders Club jijini Dar es Salaam

 Msanii nyota wa Hip Hop kutoka Marekani, Rick Ross akitumbuiza katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012 katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.
 Askari wa Kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU), akimdhibiti mmoja wa mashabiki waliohudhuria tamasha la Serengeti fiesta 2012 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.
 Msanii nyota wa Hip Hop kutoka Marekani, Rick Ross akiwa kazini.
 Ulinzi ulikuwa mkali nao ulikuwepo ili kuwadhibiti vijana wakorofi kwenye tamasha hilo.
  Msanii nyota wa Hip Hop kutoka Marekani, Rick Ross, akipiga kishoka kuukubali umati uliojitokeza kwenye onesho hilo, usiku wa kuamkia leo.
 Msanii wa Tanzania, Mwasiti Almasi (kulia), akiimba sambamba na msaani wa kundi lake.
Hapa wasanii wa nyumbani wakifanya vitu vyao katika tamasha hilo.
Msanii Diamond na wachezashoo wake wakionesha uwezo wao wa kuimba na kucheza ngoma, wakati wa tamasha hilo la Serengeti Fiesta 2012.
Hapa mashabiki wa msanii huyo wakikubali mabo ya mwanamuziki huyo wa Kimataifa wa Marekani, Rick Ross kama anavyoonekana mwanadada huyu akiwa amepagawa kabisa.
Hawa nao ilikuwa ni tabasamu tu kwenda mbele katika tamasha hilo.
Mashabiki wakipagwa na ngoma za Rick Ross wakati alipokuwa akitumbuiza sambamba na wasanii wa Tanzania kwenye tamasha hilo la Serengeti Fiesta 2012 jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. (Picha zote na mdau wetu)

No comments:

Post a Comment