TANGAZO


Tuesday, October 9, 2012

Shirika la Posta Tanzania laadhimisha Siku ya Posta Duniani, lawatunuku tuzo na zawadi wanafunzi waliofanya vizuri shindano la kuandika barua

 

 Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani, Kaimu Postamaster Mkuu, Kilala Sendama, ambaye ni Meneja Mkuu Biashara za Fedha na Utawala, akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya Posta Duniani, Dar esalaam leo. Kushoto ni Meneja Biashara ya Barua na Logistiki, Fadya Zam  na kulia ni Meneja Masoko wa Shirika, David George. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
 
Baadhi ya wakuu wa Idara na wakiwa katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Posta Duniani, Makao Makuu ya shirika hilo, Posta House, Dar es Salaam leo.

Meneja Biashara ya Barua na Logistiki, Fadya Zam, akionesha Tuzo ya Kimataifa, iliyopata Shirika la Posta Tanzania kutokana na huduma bora za Kimataifa zinazotolewa na shirika. Katikati ni Kaimu Postamaster Mkuu, ambaye ni Meneja Mkuu Biashara za Fedha na Utawala, Kilala Sendama na kulia ni Meneja Masoko, David George.
 
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani, Kaimu Postamaster Mkuu, Kilala Sendama, ambaye ni Meneja Mkuu Biashara za Fedha na Utawala, akimkabidhi Mwalimu wa Historia na Kiingereza, Sister Flora Mdoe wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Usambara ya Tanga, zawadi kutokana na shule yake kutoa mshindi wa pili katika shindano la kuandika barua.
 
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani, Kaimu Postamaster Mkuu, Kilala Sendama, ambaye ni Meneja Mkuu Biashara za Fedha na Utawala, akimkabidhi Mkuu wa Idara ya  Kiingereza wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kifungilo ya Tanga, zawadi kutokana na shule yake hiyo kutoa mshindi wa kwanza na wa tatu katika shindano la kuandika barua.
 
Mshindi wa tatu katika shindano la kuandika barua, Sonia Bernard kutoka Shule ya Kifungilo, akipokea tuzo yake kutoka kwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani, Kaimu Postamaster Mkuu, Kilala Sendama, ambaye ni Meneja Mkuu Biashara za Fedha na Utawala wakati wa hafla ya maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam leo.
 
Mshindi wa pili katika shindano la kuandika barua, Mary Spicar kutoka Shule ya Wasichana ya Usambara, akipokea tuzo yake kutoka kwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani, Kaimu Postamaster Mkuu, Kilala Sendama, ambaye ni Meneja Mkuu Biashara za Fedha na Utawala wakati wa hafla ya maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam leo.
 
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Posta duniani, Meneja Mkuu wa Biashara za Fedha na Utawala wa Shirika la Posta Tanzania, Kilala Sendama, akimkabidhi tuzo na zawadi mshindi wa kwanza wa shindano la kuandika barua kwa mchezaji kuhusu mashindano ya Olympic yaliyofanyika nchini Uingereza na jinsi anavyoyafahamu mashindano hayo, mwanafunzi Alvinar Mgoye wa Shule ya Sekondari ya wanawake ya Kifungilo, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Posta duniani, Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Meneja Biashara ya Barua na Logistiki, Fadya Zam na kushoto anayemsaidia mshindi ni Ofisa Masoko Mkuu wa shirika, Carolie Kanuti. 

 Alvinar Mgoye wa Shule ya Sekondari ya wanawake ya Kifungilo, ambaye ni mshindi wa kwanza wa kuandika barua, akiisoma barua yake hiyo wakati wa maadhimisho hayo.

Wakuu wa Idara wa Shirka la Posta Tanzania, wakipiga picha ya pamoja na washindi wa shindano la kuandika barua, Alvinar Mgoye, Mary Spicar na Sonia Bernard wakati wa hafla ya maadhimisho hayo.
 
Wazazi, walimu na viongozi wakuu wa Shirka la Posta Tanzania, wakipiga picha ya pamoja na washindi wa shindano la kuandika barua, Alvinar Mgoye, Mary Spicar na Sonia Bernard wakati wa hafla ya maadhimisho hayo.
 
Wakuu wa vitengo vya Shirika la Posta Tanzania wakipiga picha pamoja na washindi hao.

Washindi wa shindano la kuandika barua, Alvinar Mgoye, Mary Spicar na Sonia Bernard, wakipiga picha ya kumbukumbu na uongozi wa juu wa Shirika hilo, wakati wa hafla ya maadhimisho hayo.
Washindi wa shindano la kuandika barua, wa kwanza Alvinar Mgoye (kulia), wa pili Mary Spicar (katikati) na wa tatu Sonia Bernard (kushoto), wakipiga picha ya kumbukumbu huku wakionesha tuzo zao walizokabidhiwa na Shirika hilo, wakati wa hafla ya maadhimisho hayo.
 
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Posta Tanzania limefanikiwa kupata tuzo maalumu ya kimataifa kutoka kwa Umoja wa Posta Duniani (UPU).

Mbali na hilo, shirika hilo limeanzisha vituo 36 vya kutoa huduma ya Internet katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuboresha mfumo wa mawasiliano.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika Maadhimisho ya siku ya Posta duniani, Meneja Mkuu wa Biashara Tanzania Kilala Sendama alifafanua kuwa, cheti hicho kimekuja baada ya shirika kupata alama ya 1,765 kati ya alama 2000 zilizokuwa zikishindaniwa.
 
“Cheti hicho kinadhibitisha ubora wa huduma zinazotolewa na kilikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa mashirika ya posta, Yamungu Kayandabila, vile vile tuzo hiyo itatumika kama kichocheo cha kuongeza ufanisi wa mafanikio zaidi” alisema Sendama.
 
Katika hilo alichanganua kuwa licha ya shirika kukabiliwa na changamoto lukuki katika utoaji huduma endelevu, lakini limekuwa miongozi mwa historia ya mabadiliko chanya hususani katika mtandao wa dunia kuanzia ngazi ya Kitaifa pamoja na Kimataifa.
Sendama alitabanaisha kwamba mbali na tuzo hiyo, shirika limetoa tuzo kwa Wanafunzi 10 katika shule za Sekondari nchini walioshinda vizuri katika shindano la Uandishi wa Barua kwa ngazi ya kitaifa kwa mwaka 2012.
Aidha, aliwataja washindi hao ni Alvinar Mgoye kutoka shule ya sekondari Kifungilo, Mary Kilapilo sekondari ya Usambara,Sonia Chiliko Kifungilo, wote wa Mkoani Tanga, Nyinga Jackson kutoka sekondari ya Ilboru Mkoani Arusha, pamoja na Anway Omary kutoka shule ya Azania Dar es Salaam.
 
Aliwataja wengine ni Violet Richard kutoka shule ya sekondari St Joseph Mkoani Mwanza, Edith Mkwawa, Sylcheria Kaole, wote kutoka Usambara Korogwe, Raya Mwamwetta kutoka Kifungilo Mkoani Tanga, pamoja na Faraj Azizi kutoka shule ya sekondari Ummu Salama Mkoani Iringa.
 
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake waliopewa tuzo hizo, Mary Kilapilo alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi wengine kuipenda huduma hiyo kwa sababu inawapunguzia matatizo mbalimbali likiwemo la kutojiingiza katika vishawishi vya mapenzi.

No comments:

Post a Comment