Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency na Muandaaji wa Mashindano ya Miss Tanzanzia, Hashim Lundega, akitangaza mshindi wa Redd's Miss Photo Genic, ambaye ni mshiriki kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini, Lucy Stephano (katikati), wakati wa hafla ya shindano hilo, ilifanyika usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Hoteli ya E'Manyata Lodge, Monduli jijini Arusha.

Warembo walioingia kwenye tano bora wakimfurahia na kumshangilia mwenzao liyeshinda Redd's Photogenic 2012, Lucy Stephano.
Mshiriki namba 4, kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini, Lucy Stephano aliyeshinda Redd's Miss Photogenic 2012, akipozi kwa picha.
Mshiriki namba 4, kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini, Lucy Stephano, aliyeshinda Redd's Miss Photogenic 2012, akitabasamu.
Na Mwandishi Wetu, Monduli
REDD'S Miss Mbulu Lucy Stephano usiku wa kuamkia leo, alifanikiwa kukata tiketi ya kuingia 16 bora ya Redd’s Miss Tanzania, baada ya kufanikiwa kutwaa taji la Redds Miss Photogenic.
Shindano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Emanyata Lodge, uliopo mjini hapa.
Lucy, alifanikiwa kuwashinda warembo wengine 30 wanaoshiriki Redds Miss Tanzania na kufanikiwa kutwaa taji hilo.
Mrembo huyo alifanikiwa kulitwaa taji hilo, baada ya ushindani mkali uliokuwepo kati yake na Redds Miss Dar Indian Ocean, Diana Hussein na Redds Miss Ilala namba mbili, Magdalena Roy.
Kutokana na kufanikiwa kwake kutwaa taji hilo, Lucy amefanikiwa kuvuka hatua moja kubwa zaidi ya kuliwania taji la Redds Miss Tanzania linalotarajiwa kufanyika Novemba 3, mwaka huu.
Mrembo mwingine anayetarajiwa kuingia hatua hiyo atapatikana Jumamosi katika ‘Usiku wa Redd’s Miss Tanzania’ mjini Arusha pale kutakapokuwa na kinyang’ayiro cha Miss Top Model.
Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
No comments:
Post a Comment