TANGAZO


Friday, October 5, 2012

Shamra shamra za lala salama ndani ya Biafra Kinondoni leo, kuelekea kilele cha Serengeti fiesta 2012

1+(2).jpg
Mtangazaji wa Clouds FM, Dj Fetty akifanya mazungumzo na mmoja wa washindi aliyejishindia simu mapema leo jioni, viwanja vya Biafra, Kinondoni jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Ahmad Issa Michuzi)
10.jpg
Mratibu wa kikosi cha lala salama kuelekea kwenye kilele cha tamasha hilo hapo jumamosi,Mully B akitoa maelekezo mafupi kwa baadhi ya watu waliojishindia tiketi za fiesta.
2.jpg
Kama ada sehemu yenye mkusanyiko tunapeana riziki hivyo hivyo kwa namna moja ama nyingine masiha yanaendelea.
12.jpg
Mashabiki na wapenzi wa tamasha la Serengeti Fiesta wakiwa wamemzunguka kwa wingi mtangazaji Clouds FM,Dj Fetty leo kwenye viwanja vya Biafra,wakati  skwadi zima la lala salama kwenye kuelekea kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lilipotinga ndani ya viwanja hivyo na kutoa zawadi kem kem kem kwa washabiki hao,ikiwemo fedha taslim,simu,tiketi za kuingilia kwenye tamasha hilo pamoja na fulana.
7.jpg
Mussa Huseini pichani kati akiwa amezungukwa na Mashabiki/wapenzi wa tamasha la Serengeti Fiesta wakiwa wamejitokeza kwa wingi leo kwenye viwanja vya Biafra,wakati  skwadi zima la lala salama kwenye kuelekea kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lilipotinga kwenye viwanja hivyo na kutoa zawadi mbalimbali kwa washabiki hao,ikiwemo fedha taslim,simu,tiketi za kuingilia kwenye tamasha hilo pamoja na fulana.
9.jpg
Ni kushoo love tuu afuu Bhaaaaassss....!
8.jpg
Antu Mandoza akishoo love na baadhi ya mashabiki.
6.jpg
Mtangazaji wa Clouds TV,Mussa Husein akizungumza na mmoja wa mashabiki wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ndani ya viwanja vya Biafra mapema leo jioni wakati skwadi zima la lala salama kwenye kuelekea kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012 viwanjani hapo.
5.jpg
Daah hii inanitosha kabisa"
4.jpg
Hii ndio ya kwangu, ntaitinga kwa ajili ya kumuona Rozzzaaaay".
3.jpg
Mdau akiwa amepozi ni fulana yake ya fiesta mara baada ya kukabidhiwa na mwanadada Antu Mandoza ambaye ni mmoja wa watangazaji wa Clouds TV,wakiwa ndani ya viwanja vya Biafra mapema leo Kinondoni kwenye kuelekea kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
11.jpg
Ujumbe maridhawa wa kinywaji maalumu cha tamasha la Fiesta.

1.jpg
Moja ya bango yaliyosambaa kila koja ya jiji la dar na kwingineko kuhusiana na ujio mkubwa wa Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani,Rick Ross atakaetumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,litakalofanyika siku ya jumamosi,Oktoba 6 katika viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar Es salaam,Tamasha hilo pia litawahusisha wasanii mbali mbali wa hapa Tanzania. 

No comments:

Post a Comment