Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la askari shujaa katika bustani ya Confederation Square jijini Otttawa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kupokelewa katika Bunge la Seneti la Canada. Kulia ni Spika wa Bunge hilo, Mhe. Noel Kinsella, anayefuatiwa na Waziri Mkuu wa Canada, Mhe. Stephen Harper na Spika wa Bunge la wawakilishi la Canada (House of Commons), Mhe. Andrew Scheer pamoja na viongozi wengine wa bunge hilo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Waziri Mkuu wa Canada, Mhe. Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, ambapo viongozi hayo wawili walifanya mazungumzo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Canada, Mhe. Stephen Harper, wakitembea kuelekea kwenye chumba cha mkutano kuongea na wanahabari. Zulia jekundu na bendera za Canada na kiongozi wa nchi husika huwekwa sehemu hiyo, kwa heshima, wakati wa ziara ya kiongozi wa nchi ya nje aliye katika ziara rasmi nchini humo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na mabalozi wa nchi za Afrika, wanaowakilisha nchi zao nchini Canada.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa pili mbele kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Alex Massinda (mbele kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa makampuni ya Canada baada ya mazungumzo katika jengo la Rideau Hall jijini Ottawa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi toka kwa Waziri Mkuu wa Canada, Mhe. Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo. (Picha zote na Ikulu)








No comments:
Post a Comment