TANGAZO


Friday, October 5, 2012

Rais Dk. Shein apokea waya mpya wa mradi wa umeme

Waya wa Baharini, utakaotumika katika mradi wa ulazaji waya wa pili wa umeme kutoka Ras-Kiromoni, Dar es Salaam hadi Ras-Fumba Zanzibar, wenye urefu wa 37 Kilomita, katika Bandari ya Malindi, ukiwa katika meli ya Kampuni ya Viscas kutoka nchini Japan mjini Zanzibar leo. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein,  akisalimiana na Msaidizi Mtendaji Mkuu wa MCA-T kwa upande wa Zanzibar, Ahmed Rashid, alipowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja leo, kuupokea na kuukagua   waya huo wa umeme, utakaolazwa kwa siku kumi na mbili kutoka Ras-Kiromoni, Dar es Salaam hadi Ras - Fumba mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia), akisalimiana na Wahandisi wa Kampuni ya Viscas ya ulazaji waya wa umeme kutoka nchini Japan, alipowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja leo, kuupokea na kuukagua waya huo, utakaolazwa kwa siku kumi na mbili kutoka Ras-Kiromoni, Dar es Salaam hadi Ras-Fumba, mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto), akifuatana na Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati, Ramadhan Abdalla Shaaban, alipofika katika Bandari ya Malindi, Mjini Unguja leo, kuupokea na kuukagua waya wa Baharini utakaotumika katika Mradi wa ulazaji waya wa pili wa umeme
kutoka Ras-Kiromoni, Dar es Salaam hadi Ras-Fumba, mjini Zanzibar, ukiwa katika Meli ya Kampuni ya Viscas kutoka nchini Japan.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati), akipata maelezo kuhusu waya wa Baharini, utakaotumika katika Mradi wa Ulazaji waya wa pili wa Umeme kutoka Ras-Kiromoni, Dar es Salaam hadi Ras-Fumba Zanzibar, wakati alipofika katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja leo, kuupokea na
kuukagua waya huo, ukiwa katika Meli ya Kampuni ya Viscas kutoka nchini Japan.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati), akisisitiza jambo baada ya kupata maelezo kuhusu waya wa Baharini utakaotumika katika Mradi wa ulazaji waya wa pili wa umeme kutoka Ras-Kiromoni, Dar es Salaam hadi Ras-Fumba, mjini Zanzibar, wakati alipofika katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja, kuupokea na kuukagua waya huo, ukiwa katika Meli ya Kampuni ya Viscas kutoka nchini Japan.

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohd Shein, akitoka kuupokea waya Mpya wa Umeme wenye uwezo wa kuchukua Megawati 100. kutoka Tanzania Bara hadi Zanzibar, ambao umetengenezwa na Kapuni ya VISCAS COPORATION kutoka Japan. Mradi huo ni unatekelezwa na Serikali ya Marekani. (Picha za Yussuf Simai - Maelezo, Zanzibar)

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohd Shein akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika Bandari ya Zanzibar leo kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la kuwasili kwa waya mpya wa umeme, wenye uwezo wa kuchukua Megawati 100 kutoka Tanzania Bara hadi Zanzibar.

Mkurugenzi wa Shirika la umeme Zanzibar, Hassan Ali Mbarouk, akizungumza na waandishi wa habari baada ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein, kuupokea waya mpya wa umeme, wenye uwezo wa kuchukua megawati 100, kutoka Tanzania Bara hadi Zanzibar.

No comments:

Post a Comment