Meneja wa Sekta ya Kupunguza Umaskini na Kusimamia Maendeleo Ukanda wa Afrika wa Benki ya Dunia, Dk. Albert Zeufack, akiongea wakati wa mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam leo, kuhusu sekta ya Gesi asilia nchini, akiwa ameongozana na Mabalozi wa nchi kadhaa pamoja na timu ya wataalam walioletwa na washirika wa maendeleo, inayowakilisha Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za China, Uingereza na Ujerumani.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akiongea wakati wa mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam leo, kuhusu sekta ya Gesi asilia nchini. Nyuma yake mwenye laptop ni Meneja wa Sekta ya Kupunguza Umaskini na Kusimamia Maendeleo ukanda wa Afrika wa Benki ya Dunia, Dk. Albert Zeufack, akiwa ameongozana na Mabalozi wa nchi kadhaa pamoja na timu ya wataalam walioletwa na washirika wa maendeleo, inayowakilisha Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za China, Uingereza na Ujerumani.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya waandishi wa habari baada ya mkutano na wanahabari Ikulu, jijini Dar es Salaam leo kuhusu sekta ya Gesi asilia nchini. Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mabalozi wa nchi kadhaa pamoja na timu ya wataalam walioletwa na washirika wa maendeleo, inayowakilisha Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za China, Uingereza na Ujerumani. Wa pili kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Bw. Mathias Chikawe, akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzan Mlawi na maafisa waandamizi wa Ofisi ya Rais, kamati hiyo.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Makamu wa Rais Dk. Mohamed Ghalib Bilal leo, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, mara alipowasili kutoka katika ziara rasmi ya siku nne nchini Oman.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na baadhi ya wananchi waliojitokeza kumpokea leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara alipowasili kutoka katika ziara rasmi ya siku nne nchini Oman.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova leo, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara alipowasili kutoka katika ziara rasmi ya siku nne nchini Oman.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana leo, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara alipowasili kutoka katika ziara rasmi ya siku nne nchini. (Picha zote na Ikulu)
No comments:
Post a Comment