Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kushoto), akiongea na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kusisitiza utaratibu wa usajili wa magari ya umma unafuatwa na kufanyika zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote. Serikali imetoa muda hadi kufikia Novemba 15, 2012, magari ya umma yaliyo na namba za kiraia, yarejeshwe namba stahiki za magari ya umma. Baada ya hapo, operesheni hiyo itakamata magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma. Vile vile kutakuwa na aina ya namba za usajili zitakazotumika kama ST, PT, MT, JW, DFP, CW, SM na na SU. Alisema kuwa hadi sasa Serikali imesajili vyombo vya moto 123,431, yakiwemo magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma. Pichani anaefuatia mwenye sare za Polisi ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga. (Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balizi Herbert Mrango, akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kushoto), kuongea na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam, kusisitiza utaratibu wa usajili wa magari ya umma unafuatwa na kufanyika zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (kushoto), akiongea na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kusisitiza utaratibu wa usajili wa magari ya umma unafuatwa na kufanyika kwa zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (kushoto), akifafanua jambo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kusisitiza utaratibu wa usajili wa magari ya umma unafuatwa na kufanyika kwa zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (kushoto), akifafanua jambo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kusisitiza utaratibu wa usajili wa magari ya umma unafuatwa na kufanyika kwa zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (kushoto), akiteta jambo na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kusisitiza utaratibu wa usajili wa magari ya umma unafuatwa na kufanyika kwa zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (kulia), akisisitiza jambo jijini Dar es Salaam leo, wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu utaratibu wa kufuta matumizi ya namba za kiraia kwenye magari ya Serikali, taasisi na mashirika ya Umma nchini. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balizi Herbert Mrango. Serikali pia imeotoa muda hadi tarehe 15, Nov. 2012 ili magari ya umma yaliyo na namba za kiraia yarejeshwe kwenye namba stahiki za magari ya Umma kabla ya oparesheni ya kamata kamata kuanza.
No comments:
Post a Comment