TANGAZO


Friday, October 26, 2012

Rais Dk. Shein awa mgeni rasmi Baraza la Eid Zanzibar





Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi alipowasili katika Viwanja vya Salama Bwawani kuhutubia Baraza la  EID El Hajj, lililofanyika   leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akipokea salamu ya heshma ya kikosi cha polisi FFU,alipowasili katika viwanja vya Salama Bwawani Hotel,akiwa mgeni rasmi katika Baraza la EID EL HAJJ Leo.

Baadhi ya askari wa Kikosi cha Polisi cha FFU wakitoa salamu ya heshma ya Gwaride  kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, alipowasili katika viwanja vya Salama Bwawani Hotel,akiwa mgeni rasmi kulihutubia  Baraza la EID EL HAJJ Leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa,baada ya kupokea salamu ya Hesha ya gwaride la Kikosi cha Polisi FFU,leo alipowasili katika viwanja vya Salama Bwawani Hotel,akiwa mgeni rasmi kulihutubia  Baraza la EID EL HAJJ Leo.

Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa, wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu katika baraza la Eid El Hajj, huko Ukumbi wa salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar  leo.

Wananchi na waislamu wa Zanzibar, wakike na wakiume wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu katika baraza la Eid El Hajj, huko Ukumbi wa salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar leo.
 
Wananchi na waislamu wa Zanzibar, wakike na wakiume wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu katika baraza la Eid El Hajj, huko Ukumbi wa salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wananchi na waislamu wa Zanzibar katika baraza la EID El Hajj, lililofanyika katika Ukumbi wa salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar Leo.
 
Baadhi ya Wananchi na Waislamu wakijipatia vitafunio baada ya kumalizika Baraza la Eid El Hajj, lililohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee (kushoto) na Waziri wa Miundimbinu na Mawasiliano Rashid Suleiman, baada ya kulihutubia Taifa katika Baraza la Eid El Hajj Leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi na Kinamama baada ya kuwahutubia wananchi  katika Baraza la Eid El Hajj leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar. 
 
Mawaziri Wanawake wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu katika baraza la Eid El Hajj, huko Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar leo. (Picha zote na Ramadhan Othman Ikulu Zanzibar)

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar 
26.10.2012 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa ustahamilivu na uvumilivu wa Serikali umefikia kikomo kwa wale wote wanaofanya vitendo vya fujo na vurugu na itamshughulikia ipasavyo mtu yo yote atakaevunja sheria. 
Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Baraza la Idd el Hajj Lililofanyika huko katika hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar. 

Katika hotuba yake hiyo Dk. Shein alisema kuwa ustahamilivu na utulivu sio udhaifu ni heshima kubwa ya kutii amri ya MwenyeziMungu na kusisitiza kuwa hatua ya serikali kuvumilia vitendo hivyo vya uvunjifu wa amani sasa basi. ìenough is enoughî, alisisitiza Dk. Shein. 
Dk. Shein alieleza kuwa Serikali itafanya kila inavyowezekana ili kuhakikisha kwamba wanaohatarisha usalama na amani hapa ncdhini wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria zilizopo. 
Alisema kuwa Serikali itatumia sheria na taratibu zilizopo ili kuvishughulikia vitendo vya uvunjifu wa  wa amani vitakavyofanywa au kuchochewa na kikundi chochote na kusisitiza kuwa hakuna hata mtu mmoja alie juu ya sheria bali kila mtu anapaswa kufuata sheria. 

Dk. Shein alieleza kuwa  hatua za kisheria tayari zimeshaanza kuchukuliwa na tayari viongozi wanane wa Jumuiya ya UWAMSHO wamepelekewa mahakamani na wengine waliokamatw3a na polisi kwa kufanya fujo nao pia wameshafikishwa mahakamani. 

Alisema kuwa wakati huo huo Jeshi la Polisi na vyombo vya Ulinzi na Usalama vitaendelea na doria katika mitaa mbali mbali ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaishi kwa amanhi na kueleza kuwa mali za watu na maisha yao yataendelea kulindwa. 

Alieleza kuwa fujo zilizotokea Oktoba 17 mwaka huu, zilipelekea kuchomwa kwa maskani za CCM, kuvunjwa maduka, kuporwa kwa mali za watu na kuharibu miundombinu ya barabara na uharibifu mwengineo. 
Vile vile Dk. Shein alieleza kuwa fujo na vurugu hizo zilipelekea kuuliwa kwa askari wa Polisi wa kikosi cha FFU Namba F2105, Koplo Said Abdulrahman na kutoa pole kwa wafiwa, ndugu na jamaa wa marehemu. 
Alisema kuwa kiini cha fujo hizo inasadikiwa kuwa ni wafuasi wa Sheikh Farid Hadi, kiongozi wa UWAMSHO, waliodai kuwa Sheikh wao huyo haonekani na hivyo kudhania kuwa anashikiliwa na vyombo vya dola, madai ambayo hayakuwa ya kweli; 

Jeshi letu la Polisi na vyombo vya Ulinzi na Usalama viko imara katika kuvidhibiti vitendo vya fujo na vuruguÖ napenda kukuhakikishieni wananchi nyote kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti dhidi ya watakaotishia amani ya nchi yetuî,alieleza Dk. Shein. 

Aidha, Dk. Shein aliwanasihi wananchi wote kuimarisha umoja na mshikamano ambao ndio msingi mkubwa wa amani na utulivu uliopo na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaosababbisha uharibifu na kuitia hasara Serikali. 
Pamoja na hayo, Dk. Shein alisema kwua Serikali itajitahidi kuzifanyia kazi changamoto zote zilizo ndani ya uwezo wake ili kuwasideia wakulima na kuelekea katika lengo kuu la Serikali la kuimarisha sekta ya kilimo kwa lengo la kuyafanikiwa Mapinduzi ya Kilimo. 

Alitoa wito kwa wakulima na wananchi kuzitumia mvua za Vuli pale zitakaponyesha kwa ajili ya kilimo na pia, kwa ajili ya upandaji wa miti ya misitu, biashara na matunda. 

Alisisitiza pia wananchi wafuate taratibu na sheria za vitendo vinavyosababisha uharibifu wa mazingira na kuzingatia ushauri wa kitaalamu ili mazingira yawe endelevu kama ni njia moja ya kubainisha imani kwa kuwafikiria wengine. 

  Alieleza kuwa katika kukamilisha sherehe ya Idd hiyo huwa kunahimizwa kuchinja na kuwapa haki waliowajibishwa wakiwemo masikini na marafiki suna ambayo ni kiashirio cha utii alioonesha Nabii Ibrahim. 

Alieleza kwua Zanzibar imepiga hatua ya kupigiwa mfano katika maendeleo kwenye nyanja za uchumi na ustawi wa jamii tangu Mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari, 1964. Pia alieleza kuwa ripoti ya mapitio ya Dira 2020 iliyotolewa hivi karibuni inaonesha kwamba yapo mafanikio makubwa yaliopatikana. 

Mapema asubuhi Dk. Shein aliungana na waumini wengine wa dini ya Kiislamu katika sala ya Idd el Hajj iliyosaliwa katika Msikiti Mushawar, Mwembeshauri na baada ya hapo alikutana na Mashehe na viongozi mbali mbali huko Ikulu waliokwenda kumpa mkono wa Idd. 

No comments:

Post a Comment