Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa Dini ya Kiislam katika Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika kijiji cha Vuchama, Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo, ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa jiwe la msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre, leo Oktoba 26, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika kijiji cha Vuchama, Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo, ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa jiwe la msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre, leo Oktoba 26, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wananchi na waumini wa Dini ya Kiislam, wakati akiondoka katika eneo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mmoja wa waumini wa Kiislam wa kijiji cha Vuchama, wakati akiondoka eneo hilo baada ya kuzindua na kuweka jiwe la Msingi na kuchangisha fedha za ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre. leo Oktoba 26, 2012.
SERIKALI HAITAVIFUMBIA MACHO VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI
Na Joyce Anael,
Mwanga.
SERIKALI imesema haitambufimbia macho vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaotumia mwavuli wa dini kuleta vurugu zinazotishia amani na usalama wa nchi.
Makamu wa rais Dkt. Mohamed Gharib Billal, aliyasema hayo leo, wakati wa kusherehekea sikukuu ya Eid el Hajji, ambayo kitaifa imeathimishwa wilyani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza wakati akihutubia baraza la Eid, katika masjidi ya Vuchama wilyani Mwanga, mkoani Kilimanjaro Dkt. Billal alisema hivi karibuni kumeibuka wimbi la watu wanaojihusisha na vurugu za kidini ambazo chanzo chake kimekuwa ni mgogoro miongoni mwa waumini wa dini jambo ambalo linatishia amani ya nchi..
Alisema kwa kiasi kikubwa vurugu hizo zimechafua sura ya taifa na kuleta taswira mbaya kwa jamii, kutokana na uvunjifu wa amani jambo ambalo linafanywa na kikundi cha watu aliowaita wahuni.
Katika siku za hivi karibuni kumezuyka tabia mbovu za baadhi ya waumini katika misikiti kuzusha migogoro isiyo ya faida kama vile kugombea uongozi katika misikiti au kuhodhi mali za misikiti hiyo, hili ni jambo ambalo halikubaliki kabisa kwani linaleta sura mbaya katika jamii na kupelekea uvinjifu wa amani hivyo ni vema misikiti yote ikaendeshwa kwa mashauriano na makubaliano ili kuleta amani na maelewanoîalisema.
Alisema mifarakano na migogoro katika misikiti inaweza kusababisha uvunjifu wa amani na kusababisha watu washindwe kuabudu kama ilivyokusudiwa.
Naye kaimu mufti wa Tanzania sheikh Ismail Habib Makusanya,akimkaribisha makamu wa rais kutoa hotuba yake aliiomba Serikali kuharakisha uchunguzi wa vurugu ili kuweza kubaini sababu za
kuvurugika kwa amani na utulivu.
Alisema kwa kiasi kikubwa migogoro inayojitokeza hivi sasa hususani ile ya kidini ni tatizo linaloendelea kushika kasi hivyo kunahitajika jitihada za makusudi za kuzitatua.
Alisema amani inaletwa na watu wakiwemo viongozi wa dini na serikali bila kujali serikali hiyo ni ya dini ipi na serikali inatambua kuwa wajibu wake ni kuhakikisha kuwa amani inaendelea kuwepo nchini.
Aidha alisisitiza serikali kutumia vyema vyombo vyake vya dola kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya wavunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zinazostahili kwa wale watakaobainika
kuhusika na vurugu hizo.






No comments:
Post a Comment