 |
| Mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, marehemu Liberatus Barlow ukiandaliwa kushushwa toka katika gari maalum lililoubeba kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwenda nyumbani kwake kisha uwanja wa Nyamagana ambapo ibada ya kuuaga imefanyika. |
 |
| Askari wa vikosi maalum wakiulaki mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow. |
 |
| Kwa mwendo wataratibu, kikosi maalum kikiwa kimeubeba mwili wa marehemu Barlow kuupeleka mahala maalum kwa ajili ya ibada na heshima za mwisho kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa. |
 |
| Jenenza lenye mwili wa marehemu Liberatus Barlows likiwa limewekwa katika sehemu yake kwa ajili ya ibada ya kuuaga katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. |
 |
| Baadhi ya wanafamilia wakiwa kwenye hafla ya kuuaga mwili wa marehemu ndugu yao, Kamanda Barlow. |
Baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), wakiwa katika hafla hiyo jijini Mwanza leo.
 |
| Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo alisema kuwa Kamanda Barlow alikuwa ni kiongozi wa mfano na alikuwa mhimili mkubwa katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama kutokana na kutoa michango mbalimbali muhimu ya namna ya kudhibiti masuala ya uhalifu muda wote. |
 |
| Makamanda wa Jeshi la Wananchi wakiwa wamesimama kusubiri hatua inayofuata. |
 |
| Baadhi ya waombolezaji wakiwa sehemu ya jukwaa kuu la viongozi mbalimbali ndani ya uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. |
 |
| Maelfu ya wananchi wakiwa wamefurika wakati wa kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Kamanda wao. |
 |
Akiongoza misa hiyo, Paroko Raymond amesema kuwa tukio la kuuawa kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow linapasa kulaaniwa na kuwataka waumini wa dini mbalimbali kuwaombea wale waliofanya tukio hilo ili watubu kwani wamefanya kitendo ambacho sio cha kiungwana
|
 |
| Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na Uratibu, William Lukuvi akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow, katika ibada maalum iliyofanyika uwanja wa Nyamagana. |
 |
| Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo, akitoa heshima kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wake, marehemu Liberatus Barlow, aliyeuawa majuzi na watu wasiojulikana. |
 |
| Lawrance Masha ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC - CCM), Wilaya ya Nyamagana, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, marehemu Liberatus Barlow. |
 |
| Masista kutoka Parokia ya Nyakahoja wakitoa heshima zao za mwisho. |
 |
| Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku Musukuma, akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jaquline Liana wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow. |
 |
| Mbunge wa viti maaalum (CCM), Maria Hewa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kamanda Barlow. |
 |
| Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC - CCM), Wilaya ya Tarime, Christopher Gachuma akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kamanda Liberatus Barlow. |
 |
| Mbunge wa Rorya, Lameck Airo akiongoza Wabunge wenzake kuuaga mwili wa marehemu Kamanda Liberatus Barow. |
 |
| Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya uuzaji mafuta ya MOIL, Altaf Hiran Mansoor 'Dogo', akitoa heshima zake za mwisho. |
 |
| Maafisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), wakitoa heshima zao za mwisho. |
 |
| Waombolezaji wakiendelea kutoa heshima zao za mwisho |
 |
| Mfanyabiashara ambaye pia ni kada wa CCM, kata ya Kirumba, Jackson Robert (Jack Fish), akitoa heshima zake kwa mwili wa marehemu Kamanda Liberatus Barlow. |
 |
| Maafisa wa Jeshi la Wananchi, wakitoa heshima zao za mwisho. |
 |
Maafisa wa Jeshi la Wananchi, wakiendelea kutoa heshima zao za mwisho.
|
 |
Baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi wakiwa tayari kupokea amri yoyote wakati wa hafla ya kuuaga mwili wa marehemu Kamanda Barlow. Mwili wa marehemu Barlow umesafirishwa leo jioni kuelekea nyumbani kwake Ukonga jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa na ndugu na jamaa zake kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini kwake Koro, Wilaya ya Moshi Vijijini kwa ajili ya mazishi. (Picha zote na G. Sengo) |
No comments:
Post a Comment