Meneja wa Bia ya Serengeti, ambao ni wadhamini wakuu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012, Allan Chonjo akisalimiana na mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Rick Ross, mara baada ya kuwasili usiku huu, ndani ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akiwa na baadhi ya wanamuziki wenzake (pichani nyuma). Wapili kushoto ni Oparesheni Meneja wa Prime Time Promotions Ltd, Balozi Kindamba, ambao ndio waratibu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012, linalofanyika usiku huu.
Rick Ross akitoa salamu ya salut kwa mashabiki wake, waliojitokeza usiku huu (hawapo pichani) kumlaki.
Operesheni Meneja wa Prime Time Promotions, Balozi Kindamba akiwaongoza wageni wake kuelekea kwenye gari, tayari kuondoka kuelekea kwenye hoteli waliopangiwa kufikia usiku huu, kabla ya kwenda kwenye onesho la Fiesta, Viwanja vya Leaders Club. Wengine ni baadhi wanamuziki wenzake aliombatana nao.
Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Rick Ross, akiwa tayari kupanda gari kuelekea hoteli aliyopamgiwa na kisha kwenda kwenye onesho la Fiesta kwa ajili ya kutumbuiza viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na John Bukuku)
No comments:
Post a Comment