TANGAZO


Sunday, October 7, 2012

Makamu wa Rais Dk.Bilal ahitimisha matembezi ya hisani kuchangisha fedha za kujenga uwezo wa Wahandisi nchini


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki katika matembezi ya hisani ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wahandisi wa Tanzania, yaliyoandaliwa na Wahandisi hao (Local Engineers). Matembezi hayo yalianzia katika Viwanja vya Karimjee jijini na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 7, 2012. (Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR)
 Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti, Mhandisi Grace Beo, kutoka Kampuni ya Temesa ICT Engineer, akiwa ni mmoja kati ya waliochangia na kushiriki vyema katika zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wahandisi wa Tanzania, yaliyoandaliwa na Wahandisi hao (Local Engineers). Makamu alikabidhi vyeti hivyo baada ya kuhitimisha rasmi matembezi hayo ya hisani yaliyoanzia katika Viwanja vya Karimjee na kumalizikia Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 7, 2012. 
 Makamu wa Rais, Dk. Moahammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti Mhandisi Morgan Nyonyi, kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), akiwa ni mmoja kati ya waliochangia na kushiriki vyema katika zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wahandisi wa Tanzania, yaliyoandaliwa na Wahandisi hao (Local Engineers). 
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu na Wahandisi (Local Engineers), baada ya kuhitimisha matembezi hayo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Daar es Salaam leo, Oktoba 7, 2012. 

No comments:

Post a Comment