Mmoja wa wazee wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, waliohudhuria uchaguzi huo, akizungumza kusalimia wanachama kabla ya kuanza kwa mchakato huo.
Baadhi ya wanachama wapiga kura waliohudhuria uchaguzi huo, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitokea kwenye uchaguzi huo.
Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, kutoka kushoto ni Ramadhan Madabida, Chizii na John Guninita, kabla ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi huo jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na mmoja wa wasimamizi wa uchaguzi wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaa, Hadija Faraji, wakati wa uchaguzi huo, uliofanyika jana Oktoba 13, 2012, ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq, akipiga kura kumchagua Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi Mkuu wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa mchakato huo wa uchaguzi, uliofanyika Ukumbi wa PTA, Viwanja vya Sabasaba jijini jana Oktoba 13, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti mpya wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, baada ya Mwenyekiti huyo, kutangazwa rasmi kushika nafasi hiyo kwa kumshinda mpinzani wake, John Guninita kwa kura 310 kwa 214, katika uchaguzi uliofanyika jana Oktoba 13, ukumbi wa PTA, jijini Dar es Salaam.
Wasimamizi wa uchaguzi huo, wakiwa bize kuandaa utaratibu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Mwenyekiti Mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika jana Oktoba 13, 2012 kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba na kutangazwa mshindi katika kinyang’anyiri hicho, kwa kupata jumla ya kura 310, ambapo alimbwaga mpinzani wake John Guninita, aliyekuwa akitetea kiti chake, akipata kura 214. (Picha zote na OMR)
Mwenyekiti mpya wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida (kulia), akipongezwa na aliyekuwa mgombea mwenzake katika kinyang’anyiro cha uchaguzi huo, John Guninita, baada ya kutangazwa matokeo na kumsinda kwa jumla ya kura 310 kwa 214, katika uchaguzi huo, uliofanyika Ukumbi wa PTA jana Oktoba 13, 2012.
Baadhi ya wanachama wapiga kura waliohudhuria uchaguzi huo.
Mwenyekiti mpya wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika jana Oktoba 13, 2012 ukumbi wa PTA, jijini.
Sehemu ya mashabiki na wanachama wa mgombea Ramadhan Madabida wakishangilia ushindi wa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM, Mkoa wa Dar.
Baadhi ya mashabiki wa Mwenyekiti mpya wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na wanachama wa CCM, wakishangilia na kufurahia baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo, uliompa ushindi wa kiti hicho kilichokuwa kikikaliwa na aliyekuwa mpinzani wake, John Guninita.
Sehemu ya mashabiki na wanachama wa Madabida wakishangilia ushindi wa Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar, Badabida.
Mashabiki na wanachama wa CCM, wakimsindikiza Mwenyekiti mpya wa CCM, Mkoa wa Dar, Ramadhan Madabida baada ya kutangazwa mshindi katika kinyang’anyiro hicho jana.
Mashabiki na wanachama wa CCM, wakimsindikiza Mwenyekiti wao mpya wa CCM, Mkoa wa Dar, Ramadhan Madabida baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika kinyang’anyiro hicho jana.
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, aliyemaliza muda wake, John Guninita, akiondoka ukumbini hapo baada ya matokeo kutangazwa, ambapo aliyekuwa mpinzani wake, Ramadhan Madabida aliibuka kidedea.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mwanachama wa CCM, Idd Simba pamoja na baadhi ya wazee wa Chama hicho.
No comments:
Post a Comment