TANGAZO


Wednesday, October 10, 2012

Makamu wa Rais Dk. Bilal ahudhuria mkutano wa Maziwa Makuu, maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Uganda

Makamu wa Rais wa Jumhuri ya Muungano, Dk. Mohammed Gharib Bila, akihudhuria   mkutano wa tano wa viongozi wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, uliofanyia kwenye ukumbi wa Commonwealth, Hotel ya Munyonyo jijini Kamapala leo. Wengine kutoka kushoto ni Rais Paul Kagame wa Rwanda na Makamu wa Rais wa Sudan, Haji Adamu Yusufu  (Picha zote na Ofisi ya  Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal na mkewe, Mama Zakia Bilal wakifuatilia  matukio  mbalimbali  wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka50 ya Uhuru wa Uganda kwenye Uwanja wa Kololo, jijini Kampala  jana. Wengine kutoka kushoto ni Rais wa Somalia Hassan Shekhe Mahamoud  na Makamu Rais wa Sudan, Haji Adam Yusufu.


Rais Yoweri Museveni wa Uganda, akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal kwenye  sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa nchi hiyo, zilizofanyika jana kwenye Uwanja wa Kololo jijini Kampala, Uganda.


Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gaharib Bilal (wa pili kulia), akibadilishana mawazo na Rais Yoweri Museveni wa Uganda wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 50 yaUhuru wa nchi hiyo. Sherehe hizo zimefanyika jana katika Uwanja wa Kololo jijini Kampala. Wanaoonekana nyuma yao ni wake zao, Bibi Janneth Museveni (kushoto) na Mama Zakia Bilal.

No comments:

Post a Comment