TANGAZO


Sunday, October 21, 2012

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif ahutubia mkutano wa Chama chake cha CUF Buguruni, ampokea kada wa Chadema

 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, akisalimiana na viongozi wa chama hicho, wakati alipofika kwenye mkutano wa chama chake hicho, Buguruni Sheli, jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Wasanii wa Chama cha Wananchi (CUF), wanalambalamba, wakiburudisha katika mkutano wa Chama chao uliofanyika Buguruni Sheli, Dar es Salaam leo jioni.

Wananchi pamoja na wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), wakiwa kwenye mkutano wa chama hicho, Buguruni Sheli leo jioni.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, akiwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho, wakiimba wimbo wa chama chao, wakati wa mkutano uliofanyika Buguruni Sheli, jijini Dar es Salaam leo.

Wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), wakiimba wimbo wa Chama chao, wakati wa mkutano uliofanyika Buguruni Sheli leo jioni.

 Mmoja wa wanachama wa Chama cha ADC, akizungumza kwenye mkutano wa Chama chake kipya cha CUF, baada ya kujiunga rasmi na chama hicho kwenye mkutano uliofanyika Buguruni Sheli, Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Katibu Mwenezi wa CUF, Abdul Kambaya.

Baadhi ya wananchi na wanachama wa CUF, wakiwa kwenye mkutano wa Chama chao, uliofanyika Buguruni Sheli na kuhutubiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad leo jioni.

Aliyekuwa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye pia alikuwa Katibu Mwenezi wa Wanafuzi wa Vyuo Vikuu, mkoani Dodoma, Joseph Christin, akizungumza katika mkutano huo wa CUF, Buguruni Sheli leo jioni. Kulia ni Kulia ni Naibu Katibu Mwenezi wa CUF, Abdul Kambaya.

Baadhi ya wananchi na wanachama wa CUF, wakiwa kwenye mkutano wa Chama chao, uliofanyika Buguruni Sheli na kuhutubiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad leo jioni, wakifuatilia matukio mbalimbali yalioyokuwa yakifanyika kwenye mkutano huo.

Aliyekuwa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye pia alikuwa Katibu Mwenezi wa Wanafuzi wa Vyuo Vikuu, mkoani Dodoma, Joseph Christin, akivishwa sare za Chama chake kipya alichojiunga nacho, Chama cha CUF, katika mkutano uliofanyika Buguruni Sheli leo jioni.

Baadhi ya wananchi na wanachama wa CUF, wakimfurahia mwanachama huyo mpya kwenye mkutano wa Chama chao, uliofanyika Buguruni Sheli na kuhutubiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad leo jioni.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, akimpokea aliyekuwa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), aliyekuwa pia Katibu Mwenezi wa Wanafuzi wa Vyuo Vikuu, mkoani Dodoma, Joseph Christin, wakati Makamu alipokuwa katika mkutano wa Chama chake cha CUF, Buguruni, Dar es Salaam leo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, akizungumza naye mwanachama huyo mpya aliyekuwa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye pia alikuwa Katibu Mwenezi wa Wanafuzi wa Vyuo Vikuu, mkoani Dodoma, Joseph Christin, wakati Makamu alipokuwa katika mkutano wa Chama chake cha CUF, Buguruni, Dar es Salaam leo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, akimkabidhi shiti la chama hicho, liyekuwa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), aliyekuwa pia Katibu Mwenezi wa Wanafuzi wa Vyuo Vikuu, mkoani Dodoma, Joseph Christin, wakati Makamu alipokuwa katika mkutano wa Chama chake cha CUF, Buguruni, Dar es Salaam leo.

Aliyekuwa mwanachama wa Chama cha ADC, ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Ulinzi wa chama hicho, Mohamed Hassan Faki (kushoto), akirejea kwenye Chama chake cha awali cha CUF baada ya kusema kuwa alikwenda kule kwa ajili ya kukipeleleza chama hicho cha ADC.
 
Naibu Katibu Mwenezi wa CUF, Abdul Kambaya akimwelezea aliyekuwa mwanachama wa Chama cha ADC, ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Ulinzi wa chama hicho, Mohamed Hassan Faki (kushoto), aliyerejea kwenye Chama chake cha awali cha CUF baada ya kusema kuwa alikwenda kule kwa ajili ya kukipeleleza chama hicho cha ADC.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, akihutubia mkutano wa Chama chake hicho, uliofanyika, Buguruni, Dar es Salaam leo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, akihutubia mkutano wa Chama chake hicho, uliofanyika, Buguruni, Dar es Salaam leo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, akiwakabidhi wanachama wapya kadi za uanachama wa Chama hicho katika mkutano huo, uliofanyika, Buguruni, Dar es Salaam leo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, akiMkurugenzi wa Ulinzi wa CUF, Hamis Hassan (kulia), Buguruni Sheli Dar es Salaam leo.

Na Hassan Hamad (OMKR).
DAR ES SALAAM 21/10/2012.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama chake kitaendelea kutetea na kutekeleza sera yake ya kuwaunganisha watanzania popote walipo bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Amesema operesheni mchakamchaka hadi mwaka 2015 iliyozinduliwa na chama hicho hivi karibuni imekuwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera hiyo, na kwamba tayari imeanza kuleta mafanikio katika mikoa iliyoanza kutekelezwa ukiwemo mkoa wa Arusha.
 
Maalim Seif ametoa kauli hiyo katika viwanja vya Buguruni jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa chama hicho kwenye mkutano maalum wa hadhara uliolenga kuwakaribisha wanachama wapya na kuwapokea wanachama walioamua kurejea CUF baada ya kukihama na kuhamia vyama vyengine.
 
Katika mkutano huo Maalim Seif aliwapokea na kuwapa kadi za chama hicho wanachama kadhaa walioamua kurejea chama hicho wakitokea chama cha ADC wakiongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa ADC Bw. Al-Badawi.
 
Kabla ya kujiunga na ADC, Bw. Al-Badawi alikuwa mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Temeke, na sasa ameamua kurejea CUF kwa kile alichokieleza kuwa ni ubabaishaji ndani ya chama hicho kipya kinachohusishwa na mbunge wa jimbo la Wawi Mhe. Hamad Rashid Mohd.
 
Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema Tanzania imekuwa ikipita katika kipindi kigumu cha migogoro na uvunjifu wa amani, mambo ambayo yanapaswa kupigwa vita ili kurejesha hali ya amani na kuvumiliana.
 
Amedai kuwa chanzo kikuu cha migogoro ya kijamii ikiwemo ya ardhi na mizozo ya kidini inatokana na kutokuwepo kwa mikakati imara ya kuendesha nchi, na kwamba viongozi wanapaswa kujifunza kutokana na migogoro hiyo, ili kuweka mikakati imara ya kuendesha nchi kwa uhakika. 
 
“Nchi haiendeshwi kwa kuigiza, bali kwa kuwa na viongozi wenye dira ya mabadiliko kwa maendeleo ya wananchi”, alisisitiza Maalim Seif.
Amesema kutokana na viongozi kutokuwa na dira na mikakati imara ya kuendesha nchi, Watanzania wameshindwa kunufaika na rasilimali za nchi yao ambazo ni nyingi na zinaweza kuwabadilisha kiuchumi.
 
Amefafanua kuwa iwapo wananchi watanufaika moja kwa moja na rasilimali zao, wataweza kuzitunza na kuzilinda ili ziwe endelevu, na kwamba kinyume chake ni kuzihujumu rasilimali ambazo watahisi haziwanufaishi.
 
“Popote pasipo na haki hakuna amani, tunataka kila Mtanzania ajihisi kuwa ana haki sawa katika nchi hii, sio kuwa na raia wa madaraja, yaani daraja la kwanza, la pili na la tatu”, alifahamisha huku akishangaliwa na umati wa watu waliojitokeza kwenye mkutano huo.
 
Katika hatua nyengine, aliyekuwa katibu mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika tawi la Chuo Kikuu Dodoma bw. Joseph Christian amejiengua katika chama hicho na kujiunga na CUF.
 
Akizungumza katika mkutano huo bw. Joseph amesema ameamua kujiengua CHADEMA na kujiunga na CUF kwa madai kuwa chama hicho kimekuwa kikiendeshwa kwa misingi ya undugu na ukabila, na kuwatelekeza vijana wenye lengo la kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini.
 
Amewatahadhamisha vijana kuwa makini na sera za chama hicho na kuacha kukurupuka kuvamia sera za vyama wasivyovifahamu.
Nae Mwenyekiti wa ADC Wilaya ya Kinondoni Bw. Saburi Mtoro, ambaye pia ameamua kukihama chama hicho na kujiunga na CUF amemuahidi Katibu Mkuu wa CUF kuwa wanachama wote wa ADC katika Wilaya hiyo watajiunga na CUF.

No comments:

Post a Comment