TANGAZO


Saturday, October 13, 2012

Mabondia Mashali wa Tanzania, Medy wa Uganda wapima uzito tayari kuzichapa kesho





Bondia Thomas Mashali (kushoto), akitunishiana misuli na Medy Sebyala wa Uganda baada ya kupima uzito Dar es Salaam leo kwa ajili ya mpambano wao, utakaofanyika siku ya kumbukumbu ya baba wa Taifa, kesho Jumapili katika pambano la Ubingwa wa Afrika Mashariki litakalofanyika ukumbi wa Hoteli ya Friends Corner. Anayeshudia katikati ni Rais wa TPBC, Onesmo Ngowi ambaye ndiye msimamizi mkuu wa mpambano huo. (Picha zote na Super D, Mnyamwezi)



Bondia Jonas Segu akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Ibrahim Class 'King Class Mawe' kulia.



Mabondia Jonas Segu (kushoto) na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wa kitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho.



Bondia Medy Sebyala wa Uganda, akipima uzito kwa ajili ya pambano lake na Thomas Mashali (kulia), litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Hoteli ya Friends Corner jijini Dar es Salaam, pambano la Ubingwa wa Afrika Mashariki.



Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Jonas Segu (kulia), utakaofanyika kesho, likiwa ni moja ya mapambano ya utangulizi katika mpambano wa kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki kati ya Thomas Mashali na Medy Sebyala.

No comments:

Post a Comment