Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki akifungua kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa huo leo jijini. Pamoja na mambo mengine, amewataka watendaji wa Halmashauri na Manispaa za jiji, kusimamia kikamilifu matumizi sahihi ya barabara ili kuondoa tatizo la msongamano wa magari. Wengine wanaoonekana ni kushoto ni Mhe. Idd Azzan (Mb) na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa bodi hiyo, mkoani Dar es Salaam. (Picha zote na Aron Msigwa – MAELEZO)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki akifungua kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa huo leo jijini. Pamoja na mambo mengine, amewataka watendaji wa Halmashauri na Manispaa za jiji, kusimamia kikamilifu matumizi sahihi ya barabara ili kuondoa tatizo la msongamano wa magari. Wengine wanaoonekana ni kushoto ni Mhe. Idd Azzan (Mb) na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa bodi hiyo, mkoani Dar es Salaam.
Washiriki wa kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwemo Wakurugenzi wa Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa wakati wa kikao hicho leo, jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa kikao hicho, wakiwemo wabunge wa Dar es Salaam, Halima Mdee (CHADEMA) Jimbo la Kawe (wa kwanza kushoto nyuma) na Abbas Mtemvu Mbunge wa Jimbo la Temeke (CCM) wa pili kutoka kushoto mstari wa nyuma, wakifuatilia taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi na maazimio ya vikao mbalimbali vilivyofanyika.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda, akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kikao cha Bodi ya barabara kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili Manispaa ya Kinondoni ikiwemo baadhi ya watu waliojenga maeneo yasiyoruhusiwa kutumia vibaya uhuru wa Mahakama kufungua kesi na kukwamisha uendelezaji wa baadhi ya miradi ya barabara na ubomoaji wa baadhi ya nyumba zilizojengwa kinyumme cha utaratibu jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Kawe (CHADEMA), akichangia katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam leo na kutoa wito kwa watendaji wa Halmashauri kusimamia ipasavyo makusanyo ya fedha ili kuziwezesha Halmashauri kuboresha miundombinu jijini.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke Bi. Magreth Nyalile, akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na washiriki wa kikao hicho, wakiwemo Wabunge kuhusu hatua zinazochukuliwa na Halmashauri ya Temeke kujenga miundombinu na maegesho yatakayotumiwa na malori yanayotoka bandarini na kupunguza kero kwa watumiaji wengine wa barabara hizo, kutokana na kushindwa kupitika kutokana na msongamano wa malori hayo.








No comments:
Post a Comment