TANGAZO


Thursday, October 4, 2012

Wajumbe Tume ya Mabadiliko ya Katiba watembelea vitengo vya Sekretarieti ya Tume

Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Hanifa Masaninga (kushoto) akitoa ufafanuzi namna ya sauti zenye maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya zinavyopekelewa katika Makao Makuu ya Tume Jijini Dar es Salaam kwa wajumbe wa Tume hiyo wakati wa ziara ya kutembelea vitengo mbalimbali vilivyopo katika Tume hiyo jana Jumatano tarehe 3. Oktoba, 2012. Kutoka kulia ni wajumbe wa Tume hao, Mwantumu Malale (kulia), Maria Kashonda (aliyekaa), Riziki Ngwali (wa pili kulia), Joseph Butiku (wa tatu kulia), Yahya Msulwa (wa tatu kushoto) na wa pili kushoto ni Katibu wa Tume, Assaa Rashid.


Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mohamed Khamis Hamad (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu kazi za uchambuzi wa maoni ya wananchi wakati wa ziara ya wajumbe hao waliotembelea vitengo mbalimbali vya Sekretarieti ya Tume hiyo jana Jumatano tarehe 3. Oktoba,2012. Kushoto ni Mjumbe wa Tume hiyo, Humphery Polepole na wa pili kushoto ni Mjumbe mwingine, Suleiman Ali.


Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Hanifa Masaninga (kushoto) akiwaeleza Wajumbe wa Tume hiyo namna ya sauti zenye maoni ya wananchi zinavyoweza kupokelewa katika Makao Makuu ya Tume hiyo Jijini Dar es Salaam wakati wajumbe hao walipofanya ziara ya kutembelea vitengo mbalimbali vilivyopo katika Sekretarieti ya Tume hiyo jana Jumatano tarehe 3. Oktoba, 2012. Kutoka kulia ni Dkt. Edmund Mvungi, Jesca Mkuchu (wa pili kulia), Simai Said (wa pili kulia) na mstari nyuma (kushoto) ni Katibu wa Tume Assaa Rashid na wa pili kushoto ni Mjumbe wa Tume, Esther Mkwizu.


 Mujmbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mohamed Khamis Hamad akiwaeleza Wajumbe wa Tume hiyo kuhusu kazi za uchambuzi wa maoni ya wananchi wakati wa ziara ya wajumbe hao waliotembelea vitengo mbalimbali vilivyopo katika Sekretarieti ya Tume hiyo Jijini Dar es Salaam jana Jumatano tarehe 3. Oktoba, 2012.  Kushoto ni Mjumbe wa Tume, Esther Mkwizu, Omary Mussa katikati na Simai Said (wa pili kulia). 



Wajumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mwantumu Malale (kulia), Maria Kashonda (aliyekaa), Riziki Ngwali (wa pili kulia), Joseph Butiku (wa tatu kulia) na Yahya Msulwa (wa tatu kushoto) wakitazama namna sauti zenye maoni ya wananchi zinavyopokelewa katika Makao Makuu ya Tume Jijini Dar es Salaam kutoka katika  mikutano inayoitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Mikoa mbalimbali nchini wakati wa ziara ya wajumbe hao jana Jumatano tarehe 3. Oktoba, 2012. Kushoto ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume hiyo, Hanifa Masaninga na (wa pili kushoto) ni Katibu wa Tume, Assaa Rashid. (Picha zote na Tume ya Katiba)

No comments:

Post a Comment