TANGAZO


Sunday, October 14, 2012

Drogba aponea chupuchupu kudundwa, askari wamwokoa, mashabiki Senegal wa vunja mchezo kupinga Penalti


 Askari wa Jeshi la Polisi wa Senegal, wakimlinda nyota wa Ivory Coast Didier Drogba, asipigwe na mashabiki waliokuwa wakipinga maamuzi ya penati yake aliyofunga dakika ya 72 ya pambano la kuwania kufuzu AFCON 2013 dhidi ya Senegal. Mechi ilivunjika kwa vurugu hizo dakika ya 76, huku Ivory Coast ikiwa mbele kwa mabao 2-0.
 Sio Drogba peke yake, nyota wote wa Ivory Coast wakaingia majaribuni, na hapa wanaonekana wakitolewa kwa mafungu kuingia vyumbani chini ya ulinzi kuokoa maisha yao. Jezi namba 4 ni Kolo Toure.
Askari wakiwatoa chini ya ulinzi wachezaji wa Ivory Coast na waamuzi akiwamo Slim Jedid wa Tunisia, baada ya vurugu kuzuka kupinga penati tata ya mwamuzi huyo kwenye Uwanja wa Leopold Senghor jijini Dakar.
 Hali haikuwa salama jukwaani, kwani mashabiki wa Simba wa Teranga walifanya vurugu kubwa na kuchoma vitu kama wanavyoonekana wakitawanyika baada ya kurushiwa mabomu ya machozi na askari wa kutuliza ghasia.
Vurugu zote zilianzia hapa. Drogba akiitendea haki penati ya mwamuzi Slim Jedid na kufunga bao la pili na kuzima ndoto za Senegal kuibuka na ushindi na kufuzu AFCON 2013. Drogba ndiye aliyefunga bao la kwanza la Tembo wa Ivory Coast.

DAKAR, Senagal
Wachezaji wa Manchester City, Kolo na nduguye Yaya Toure, nyota wa Newcastle Cheick Tiote na mshambuliaji wa Arsenal, Gervinho – walikuwa ni miongoni mwa nyota wa Ivory Coast waliolengwa na mshambulizi ya mashabiki hao

MSHAMBULIAJI Didier Drogba wa Ivory Coast, jana usiku alikuwa kwenye wakati mgumu baada ya kuvamiwa na mashabiki soka nchini Senegal katika mechi ya kuwania kufuzu Mataifa Afrika 2013.

Nyota huyo wa zamani wa Chelsea, alifunga mara mbili kipindi cha pili, ikiwamo penati iliyozua ghasia kubwa aliyofunga dakika ya 71 na kukasirisha mashabiki wa Simba wa Teranga waliovamia uwanja na kumlazimu mwamuzi kuvunja pambano.

Vikosi vya kutuliza ghasia vya jeshi la polisi na walinzi binafsi wakafanikiwa kumlinda Drogba na kumuweka mikononi mwao – lakini wakati huo tayari alishapata purukushani kutoka kwa mashabiki hao.

Wachezaji wa Manchester City, Kolo na nduguye Yaya Toure, nyota wa Newcastle Cheick Tiote na mshambuliaji wa Arsenal, Gervinho – walikuwa ni miongoni mwa nyota wa Ivory Coast waliolengwa na mshambulizi ya mashabiki hao kutokea jukwaani.

Lakini taarifa kutoka Etihad yaliko makazi ya Man City klabu ya Kolo na Yaya Toure, ilithibitisha kuingia matatani kwa nyota wao na kuongeza: “Taarifa za awali zimetufikia kwamba wanandugu hao hawakudhulika katika ghasia hizo.”

Iliongeza kuwa: “Vurugu zilitokana na Didier Drogba kutumbukiza nyavuni penati na kuipa Elephants uongozi wa mabao 2-0, ambapo mashabiki walikasirishwa na mazingira tatanishi ya penati iliyotolewa na mwamuzi Slim Jedid wa Tunisia kwenye Uwanja wa Leopold Senghor jijini hapa.

“Miali ya moto (fataki), vyupa na vitu vingine vikaanza kurushwa kutokea jukwaani kuwalenga wachezaji, huku wengine wakivamia uwanja mwishoni mwa mchezo.”

Bao la pili la Drogba katika ushindi huo wa 2-0, uliifanya Ivory Coast kuwa mbele na hatimaye kuitoa Senegal kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-2, lakini sherehe za wachezaji wa Elephant kushangilia ushindi zikageuka janga kutokana na vurugu hizo.

Mashabiki hao wa Senegal wakaahamishi hasira zao majukwaani kwa kuchoma vitu, kusababisha moshi mwingi angani kuufunika uwanja huyo na kumlazimu Jedid kulivunja pambano hilo dakika ya 76.

Polisi wakafanya kazi ya ziada kuwanusuru mashabiki wa Ivory Coast kwa kuwakusanya katikati ya uwanja – na kuwatorosha kutoka uwanjani hapo kwa magario maalum, huku ikiwatawanya wakle wa Senegal kwa mabomu ya machozi.

Vikosi vya usalama uwanjani hapo havikuishia hapo, bali vilifanya kazi ya ziada kuwalinda nyota wa Senegal waliokuwa kwenye hatari ya kuingia matatizoni, wakiwamo Demba Ba na Papiss Cisse wa Newcastle, na nyota wa West Ham Mohamed Diame.

No comments:

Post a Comment