TANGAZO


Wednesday, October 3, 2012

CRDB yafungua tawi jipya Chamwino, Dodoma


Ofisa Mauzo wa CRDB, Tawi la Chamwino Dodoma, Moses Wamela, akihudumia wateja wanaojiunga na huduma ya SIM Banking. (Picha zote na Mpiga Picha Wetu)
 
Ofisa Mauzo wa CRDB, Tawi la Chamwino Dodoma, Moses Wamela, akihudumia wateja wanaojiunga na huduma ya SIM Banking tawini hapo leo.
 
Ofisa Mauzo wa CRDB, Tawi la Chamwino, Moses Wamela akioonesha namna ya huduma ya SIM Banking inavyofanya kazi.
 
DODOMA, Tanzania
BENKI CRDB nchini, imefungua lake Tawi Jipya la Chamwino katikati ya Mji Mkuu wa Tanzania Dodoma, ili kusogeza huduma zake karibu na wateja wake.
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Ofisa Mauzo Willy Kamwela alisema, nia ya CRDB kufungua tawi hilo hivi karibuni ni kuwahakikishia wateja wake mkoani Dodoma na wanafunzi kuwa wanawajali.
“Tawi hili lina huduma zote muhimu kama yalivyo matawi mengine nchini, zikiwamo huduma na SIM Banking, Tembo Card, Master Card, kadi za kuchukulia fedha kimataifa za VISA na mikopo mbalimbali," alisema Kamwela.
Kamwela alisema kuwa, tawi la Chamwino lenye ATM mbili ni miongoni mwa matawi 10 na huduma 75 za mtandao na huduma 230 za ATM ikiwamo huduma ya SIM Banking zilizoko nchini zilizoimarishwa tangu 1990.
Mbali ya CRDB kuwa kitovu cha Elimu, Uchumi na Biashara, kwa sasa ina wateja zaidi ya Milioni moja inajivunia kuwa na mali za mtaji wa shilingi trioni tatu, ambapo wananchi wameipongeza CRDB kwa ufunguzi wa tawi hilo mpya.
Aidha Meneja wa Tawi hilo la CRDB Chamwino Peter Chambua, amewataka wateja wao kumiminika kupata huduma za SIM Card, ATM na kuomba mikopo ili kuendana na zama hizi Sayansi na Teknolojia, ili kujipatia maendeleo yaliyokusudiwa.

No comments:

Post a Comment