TANGAZO


Tuesday, October 23, 2012

Chama cha ADC chafanya mkutano jijini Mwanza

Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC), Lucas Kadawi Limbu (mwenye suti katikati), akiwapungia mkono wafuasi wa chama hicho, baada ya kukagua kikundi cha ngoma muda mfupi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza mwishoni mwa wiki. Limbu alifanya mkutano wa hadhara na kupokea wanachama wapya katika Kata ya Igoma jijini humo. Kushoto ni Kamishna wa chama hicho, Kanda ya Ziwa, Shaaban Itutu.

Katibu Mkuu wa ADC, Lucas Kadawi Limbu (mwenye tai nyekundu), akisamilia wafuasi wa chama hicho, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Mwanza, kabla ya kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika Kata ya Igoma, ambapo wananchama wapatao 1,300 walijunga na chama hicho. Kushoto ni Kamishna wa Chama hicho, Kanda ya Ziwa, Shaaban Itutu.

Waendesha pikipiki wakiongoza mapokezi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC), Lucas  Kadawi Limbu, alipowasili jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi na baadaye kufanya mkutano wa hadhara katika Kata ya Igoma, jijini Mwanza mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katibu Mkuu wa Chama cha Democratic For Change (ADC), akihutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Igoma, jijini Mwanza.

Katibu Mkuu wa Chama cha Democratic For Change (ADC), akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Igoma, jijini Mwanza.
Wananchi wa Kata ya Igoma, wakigombea kadi za Chama cha Alliance For Democratic For Change (ADC), kutoka kwa Katibu Mkuu wa chanma hicho), Lucas Kadawi Limbu, (mwenye suti), wakati wa mkutano wa chama hicho mwishoni mwa wiki iliyopita.  Wanachama wapya wapatao 1300, walijiunga na chama hicho. (Picha zote na Baltazar Mashaka)

No comments:

Post a Comment