Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini Dk. Aloyce Nzuki (kushoto), akimtambulisha mpishi maarufu duniani kutoka nchini India, Sanjeev Kapoor kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), leo jijini Dar es Salaam, ambaye amekuja nchini kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini. Mpishi Kapoor Atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi hivyo. (Picha zote na Anna Nkinda – Maelezo) Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini, Dk. Aloyce Nzuki (wa pili kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na mpishi maarufu duniani kutoka nchini India, Sanjeev Kapoor (wa pili kulia), mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina yao na waandishi wa habari, uliohusu umuhimu wa vyakula vya asili katika sekta ya utalii, uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Meneja Mkuu wa Hoteli ya Serena, Daniel Sambai na kushoto ni Mkurungezi wa Performance Ltd Tanzania, Runjiv Kapur.Baadhi wa wageni waalikwa na mwaandishi wa habari, wakimsiliza mpishi maarufu duniani kutoka nchini India, Sanjeev Kapoor (hayupo pichani), akielezea umuhimu wa vyakula vya asili katika sekta ya utalii wa nchi. Mpishi Kapoor atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga, ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini.
No comments:
Post a Comment